


Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
WAZIRI wa Elimu ,Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda amesema Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa la Elimu ‘elearning’ Afrika linalotarajiwa kufanyika Mei 07 hadi 09, 2025 katika kituo cha mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar Es salaam.
Aidha kauli mbiu ya kongamano hilo ni ‘kufikilia upya Elimu,na maendeleo ya raslimali watu kwa ustawi wa Afrika’
Prof. Mkenda,ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma ambapo amesema , zaidi ya nchi 65 za Afrika zitashiriki kongamano hilo kwa ajili ya kujadili,kubadilishana uzoefu,kuhamasisha uwekezaji na kuazimia mipango ya pamoja ya kuchagiza matumizi ya Teknolojia za kidijitali katika sekta ya Elimu barani Afrika.
“Kongamaono la 18 la elearning afrika litafanyika katika kituo cha kimataifa cha Julius Nyerere jijini dar es salaam kuanzia mei 07 hadi 09 mwaka huu,tangu kuasisiwa kwake mwaka 2005 kongamano hili lishafanyika nchi 17 ikiwemo Tanzania.
Aidha alisema Kongamano kama hilo lilifanyika hapa nchini 2021 hivyo mwaka huu litakuwa linafanyika kwa mara ya pili.
“Kongamano hili linalenga kuwakutanisha wadau zaidi ya 1500 kutoka zaidi ya 65 barani Afrika”,alisema Prof.Mkenda
Aidha Prof.Mkenda amesema makundi hayo ya wadau yatajumuisha watunga sera,watoa maamuzi,wataalamu wa Elimu,wataalamu wa Teknolojia,watafiti,wabunifu,wafanya biashara,wawekezaji na wadau wa maendeleo.
Hata hivyo amesema kongamano hilo litajumuisha mkutano wa mawaziri zaidi ya 50 kutoka nchi 49 barani Afrika utakao kuwa na lengo la kuazimia mikakati ya pamoja na kuandaa nguvu kazi mahiri katika kubuni, kuzalisha,na kuimalisha matumizi ya kidigitali.
“Kama wenyeji wa kongamano hili nchi yetu inatarajia kunufaika na fursa mbalimbali kutokana na kuwa mwenyeji wa kongamano hili ambapo tutabaini mikakati mpya hususani katika sekta ya Elimu”,amesema
More Stories
Mkandarasi atakiwa kujenga haraka daraja la muda Bonyokwa
Rais Samia atoa msaada kwa kituo kinachohifadhi wasichana waliokimbia ukatili
Mo Dewji na Urithi anaoujenga ,unavyoenda mbali zaidi ya mafanikio binafsi