Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
ALFIRDAUS foundation yaandaa kongamano la kwanza la vijana wa kiislamu kufanyika nchini Tanzania Novemba 10, 2024 lililowashirikisha vijana wa kada mbalimbali waume kwa wake wakiwemo mashekh na wanazuoni.
Katika hafla hiyo palikuwa na Tuzo mbalimbali zilizoitwa kwa jina la Tameya awards ambazo walipatiwa washindi kutokana na vigezo.mgeni rasmi katika sherehe hiyo alikuwa shekh wa mkoa wa Dar es salaam shekh Walid ambaye alimuwakilisha Mufti wa Tanzania Shekh Abubakari Zuberi.
Miongoni mwa vijana saba (7) waliopata bahati ya kupata Tuzo hizo katika hatua ya awali ni pamoja na Kassimu Mrisho, Omari Juma, Omari Baajuni , Ibrahim Omary , Ibrahim Hussein, Halima Shabuge na Azza Seleman
Akizungumza jijini Dar es salaam katika ukumbi wa mwalimu Nyerere shekh Alhad Walidi amesema Tuzo hizo zinawaheshimisha vijana wa kiislamu kutambua majukumu yao katika kuendeleza dini ya mwenyezimungu.
“Tuzo hizi ni muhimu kwa ajili ya vijana wetu wa kiislamu kutambua amani na ushirikiano ni kitu muhimu, vijana ndio tegemeo kubwa la dini yetu ambapo mtume wetu Muhammad aliwasifu vijana na kuwajengea misingi Bora hivyo nasi tunawajibu wa kuwajengea vijana wetu kwenye misingi Bora,” amesema Shekh Walid
Aliendelea kusema vijana watumike vema katika umma wa kiislamu Ili kuwa wamoja katika kuimarisha dini yao na mambo yao ya msingi katika kuunufaisha umma wa kiislamu duniani kote.
Aidha Tuzo hizo za Tameya zililenga zaidi kwenye maeneo ya afya , kutangaza dini ya kiislamu , vijana kushirikiana katika masuala ya kijamii, biashara, kiteknolojia , sanaa na maadili mbalimbali.
Kwa upande wake Alfirdaus Chartable Foundation muandaaji wa tuzo hizo amesema kuwa lengo la Tuzo hizo ni kuwapa fursa vijana wetu wa kiislamu wa moja katika kujisimamia dini yetu lakini kutoa fursa ya kujiendeleza katika ulimwengu wa sayansi na teknolojia.
More Stories
The Desk & Chair yashusha neema Gereza la Butimba
TVLA,yapongezwa kwa kuzalisha chanjo
TAKUKURU,yasaidia kurejesha hekali 8