Na Penina Malundo, TimesMajira Online, Morogoro
MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba(TMDA) imesema kwa mwaka wa fedha 2019/2020 takribani Kondomu Paketi 17,076 zimeondolewa sokoni kutokana na kutokidhi viwango vya ubora.

Akizungumza leo, Kaimu Mkurugenzi wa Dawa na vifaa Tiba, Akida Khea wakati wa kujibu maswali ya waandishi wa habari katika kikao kazi cha uhamasishaji wa waandishi wa habari kuhusu usimamizi wa Sheria ya Dawa na Vifaa Tiba sura 219, mkoani Morogoro.
Amesema bidhaa hizo zilizoondolewa ni zile feki ambazo hazikidhi matakwa ya viwango zinazoweza kuwa na madhara na nyingine ni zile ambazo zilikuwa zikiuzwa kwa kutumia jina la mtu mwingine.
Kondomu hizo zilizoondolewa sokoni ni takribani aina tano ambazo ni Life Guard, Ultimate, Maximum Classic, Prudence na Chishango.
More Stories
Huduma ya kusafisha figo yasogezwa Manyara
Rais Samia aandika historia barani Afrika
Mapambano dhidi ya Marburg waandishi watakiwa kuelimisha jamii