Na Mwandishi Wetu, Timesmajira
Kocha Mkuu wa US Monastir, Darko Novic ametoa kauli ya mitego kuwa hawatatumia nguvu nyingi watakapovaana na Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Yanga SC.
Miamba hiyo itakutana kesho Jumapili, katika mchezo wa mzunguuko watano wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika, kwenye Uwanja wa Bengamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
Akiweka wazi hilo Kocha Darko Novic amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo huo, lakini hatatumia nguvu kubwa, kwani tayari wameshafuzu Robo Fainali hivyo hawatawatumia wachezaji wao muhimu na tegemeo kwa lengo la kupata majeraha wakati wana kibarua kigumu mbele ya safari.
“Hatukuja Tanzania kutafuta alama tatu wala suluhu kwa sababu tumeshafuzu Robo Fainali, hivyo tutacheza mpira wa kawaida bila ya kutumia nguvu nyingi kama tulivyocheza nao Tunisia.
“Tunafahamu wapinzani wetu wanahitaji ushindi ili wafuzu hatua inayofuatia ya Robo, hivyo tayari nimewaambia wachezaji wacheze kwa makini ili wamalize mchezo huo bila ya majeraha yoyote.”
“Kwani tuna kibarua kigumu mbele ya safari ndefu katika michuano hii, malengo yetu ni kufika fainali hivyo sitaki kuona wakipatikana majeruhi katika mchezo huu,” amesema Darko Novic.
More Stories
Samia awazawadi Stars milioni 700/-
Samia atoa bilioni 8/- kukarabati viwanja vya CHAN, AFCON
Rasmi Chatsoko mdhamini mkuu wa Goba Hills Marathon 2025