LIVERPOOL, England
Kocha Mkuu wa klabu ya Liverpool Jurgen Klopp, amewapa pongezi wachezaji wake baada ya kupambana muda wote katika mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Chelsea na kufnikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0, mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia leo kwenye dimba la Stamford Bridg, Uingereza.
Huo ulikuwa mchezo wa pili wa Ligi Kuu England kwa Liverpool kushinda baada ya kuanza kuifunga Leeds mabao 4-0, ulichezwa kwenye Uwanja wa Stamford Bridge.
Mabao ya ushindi kwa Liverpool yalipatikana dakika ya 50 na 54 huku mtupiaji akiwa Sadio Mane, raia wa Senegal ambaye aliwamaliza kabisa Chelsea wakiwa kwenye Uwanja wao wa nyumbani.
Mara baada ya mchezo huo kumalizika kocha wa Liverpool Jurgen Klopp alisema, amefurahishwa na kasi waliyoionesha kipindi chote cha dakika 90 na jinsi walivyopambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri.
“Nilifurahishwa na kasi walioionesha wachezaji wangu kipindi chote na namna ambavyo walipambana kusaka matokeo,” alisema Klopp.
More Stories
15 wajinoa Juventus,akiwemo mtoto wa Mwenyekiti wa CCM Mbeya
Za Kwetu Fashion Show, yawapaisha wanamitindo nchini
TCAA yaadhimisha siku ya usafiri wa anga Duniani kwa kushiriki mbio za Marathon UDSM