Na Mwandishi wetu Timesmajira
MSIMU wa tatu wa KnockOut ya mama uliopo chini ya Kampuni ya Mafia Boxing Promotion unatarajia kufanyika Februari 28 mwaka huu Jijini Dar es salaam katika ukumbi wa magomeni sokoni huku ukipambwa na mapambano 12.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mafia Boxing Promotion Ally Zayumba wakati akizugumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam mapema leo Februari 25, 2025.
Amesema lengo la mapambano hayo ni kunadi miradi iliyotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
“Usiku huo pambano kuu litakuwa ni la Bondia Amiri Matumla ambaye atapanda ulingoni katika Ukumbi wa Magomeni Sokoni kuzichapa dhidi ya mpinzani wake kutoka Namibia, Paul Amavila”amesema
Nakuongeza kuwa
“Bondia Matumla katika pambano hilo atazichapa na mpinzani wake huyo kwa mizunguko nane”amesema
Aidha amesema mapambano mengine 11 ya utangulizi yataongozwa na mkongwe Dullah Mbabe huku baadhi ya mabondia wengine watakaopanda ulingoni wakiwa ni Oscar Richard atakayezipiga na bondia kutoka Malawi.
Wengine ni Rashid Mtange kutoka Nacoz Camp chini ya kocha Ramadhani Uhadi ‘Rama Jah’ atazichapa na bondia kutoka India na wengineo.
Aidha amesema Mchezo wa ngumi katika kipindi hiki cha uongozi wa Rais Dkt Samia, umekuwa na mafanikio makubwa hivyo ni vema watanzania wakaendelea kumuunga mkono.
Kwa upande wa viingilio katika usiku huo wa Knock Out ya Mama Msimu wa tatu amesema vitakuwa ni shilingi, 50,000, sh. 20000 na 10,000
Naye Msanii maarufu Sheta ambaye ni balozi wa tukio hilo Nurdini Bilal amesema mchezo wa ngumi ni burudani inayosaidia mawazo na pia ni chanzo cha ajira kwa mabondia.
Kwa upande wake, bondia Amiri Matumla, ambaye anapigana kwa mara ya kwanza katika pambano la kimataifa, ameishukuru Mafia Boxing Promotion kwa kumpokea na ameahidi kufanya vizuri katika safari yake ya masumbwi.
More Stories
CCM yaombwa kuchunguza vitendo vinavyofanywa na Mwenyekiti wa CCM Rorya
Rais Samia ataka watumishi kumaliza adha ya maji kwa wananchi
Serikali, wadau waombwa kusapoti mashindano ya Lina PG Tour