Klabu ya KMC imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu wa 2020-21 baada ya kumnasa aliyekuwa beki wa kati wa Lipuli David Mwasa. Beki huyo alikuwa ni nguzo muhimu kwa Lipuli hasa msimu uliomalizikaÂ
Nyota huyo amelamba mkataba mnono wa kuichezea timu hiyo kwa miaka miwili.Uongozi wa KMC umeendelea kuimarisha eneo la ulinzi baada ya juzi kumsajili aliyekuwa beki wa Yanga Vicente Chikupe maarufu kwa jina la Dante na sasa wameongeza nguvu kwa kumsajili Mwasa.
Ukuta wa KMC unategemewa kuwa imara kwani mabeki hao wote wawili ni imara sana na hii itaongeza changamoto kwenye ligi
More Stories
Kasulu FC mabingwa mashindano Khimji 2025
Fainali Khimji cup kufanyika Februari 7,2025
Naibu Waziri wa Fedha abariki ujio mpya wa Bahati Nasibu