Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Mshtakiwa Pinisto Antony Nzali akisindikizwa na Askari kuingia kusomewa mashitaka matatu yanayomkabiri baada ya kutengeneza Video inayomuonyesha Raisi Samia Suluhu Hassani akiimba na nyingine ikimuonyesha Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete.
Mashitaka hayo yamesomwa na wakili wa serikari Slyvia Mitanto mbele ya Hakimu Mkazi kisutu Pamela Mazengo hii Leo November 10 mwaka huu.
Katika hati ya mashitaka imeeleza mnamo October 8 mwaka huu mtuhumiwa akiwa ndani ya jamhuri ya muungano wa Tanzania kupitia mtandao wa TikTok alimchafua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kutuma video inayomuonyesha Rais akiimba wakati sio kweli.
Pia mnamo October 10 mwaka huu alichapisha video nyingine ikimuonyesha Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete akiwa anaimba wakati sio kweli.
Katika shitaka la Tatu anakabiliwa na shitaka la kushindwa kusajili SIM kadi ambayo mwanzo ilisajiliwa Kwa jina la mtu mwingine.
Baada ya mtuhumiwa kuulizwa na hakimu mazengo kuhusu tuhuma hizo amekana kutenda, hivyo Kesi hiyo imehairiswa hadi kesho November 11 mwaka 2022 na Mtuhumiwa Karudishwa rumande.
More Stories
Wakuu wa Wilaya,Wakurugenzi watakiwa kusimamia programu za chakula shuleni
Mbowe akuna wengi kuhusu maridhiano
Waziri Chana amuapisha Kamishna uhifadhi NCAA, ampa maagizo mazito