December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kizimbani kwa kuisababishia serikali hasara ya shilingi milioni 487

Na Irene Fundi, TimesMajira Online

WAKAZI wa Dar es salaam Erasto Anthony Dewa(54), Ramadhani Jabili Salumu (24) na Frank Ngata (35), wamefikishwa kizimbani mahakama ya hakimu mkazi kisutu Kwa kusababishia serikali hasara ya shilingi milioni 487.

Shitaka hilo limesimwa na wakili mwandamizi wa TRA Medalakini Emmanuel hapo Jana mbele ya Hakimu mkazi mwandamizi kisutu Francis mhina.

Katika hati ya mashitaka imedaiwa kuwa Septemba 2022 katika eneo la tabata ndani ya Ilala daresalaam kwa pamoja na kwa kitendo chao cha makusudi Cha kukwepa kulipa kodi kwa njia ya ulaghai waliisababishia serikari hasara ya shilingi 487,945,210.

Emanuel ameieleza mahakama kuwa watuhumiwa wanakabiliwa na mashitaka matatu na shitaka Moja linamkabili Erasto Antony Dewa meneja wa Kampuni ya Dewa trending.

Katika shitaka la kwanza imeelezwa kuwa watuhumiwa Kwa pamoja walihusika kutoka taarifa za uongo kuwa shehena ya marobota ya shuka yalikuwa yanasafirishwa kwenda Malawi lakini walilitelekeza shehena Hilo tabata.

Ikiwa shitaka la pili ni kufanya ulaghai wa kuchepusha bidhaa za vitenge kutoka njia iliyotengwa ya daresalaam kwenda Malawi ambapo mzigo huo ulipakuliwa katika eneo la tabata wilaya ya Ilalakatika.

Shitaka la Tatu linamkabili Erasto Antony Dewa Kwa kutoa maelezo ya uongo ya shehena la maroba 290 kama mashuka badara ya vitenge.

Pia shitaka la nne linawakabili watuhumiwa wote ambapo wanatuhumiwa Kwa kuisababishia asara serikari ya zaidi ya shilingi milioni 487.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo hakimu mhina amesema kutokana na kosa la kukwepa kulipwa Kodi ni makosa ya uhujumu uchumi hivyo watuhumiwa hawakutakiwa kujibu chochote watuhumiwa wamerudishwa maabusu.

Kesi hiyo imehairiswa hadi Novemba 24 mwaka huu kwaajiri ya kutajwa upya.