December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kiwanda cha GF vehicles chatengeneza Magari 100

Na Angela Mazula,TimesMajira Online.

KIWANDA kipya cha kutengeneza magari nchini Tanzania GF vehicles Assemblers (GFA), kilichopo Kibaha mkoani Pwani kimetimiza utengenezaji wa magari 100 tangu kilipoanza kazi rasmi mwezi January mwaka huu.

Akizungumza katika sherehe za kuruhusu magari hayo 100 kuanza kutumika mara tuu baada ya kuunganishwa, Meneja mkuu wa kiwanda hicho Ezra Mereng amesema, ni kazi ngumu kukamilisha zoezi la uunganishaji na utengenezaji wa magari hayo kwa kuwa Tanzania ndio Kiwanda cha kwanza kutengeneza na kuunganisha magari ambayo yameanza hivi karibuni.

Hata hivyo, amezungummzia changamoto ambazo wamekutana nazo, kuwa kutokuwa na wataalamu wengi katika sekta hiyo ya Magari lakini kwa kushirikiana na wataalamu wa nje wameunganisha magari 10 ya awali na baadae wakaondoka na kubaki na watanzani na kufanikiwa kumaliza magari 100 ya awamu ya kwanza.

Amezitaka tasisisi za Serikali kuanza kuagiza magari ambayo hayajaunganishwa na kazi ya kuunganisha ifanyike katika viwanda vya ndani ili kukuza pato la taifa na kuweza kuongeza ajira kwa watanzania ili nchi ipate fedha za kigeni kwa kuuza magari hayo nchi9 jirani.

Nae Afisa Masoko na manunuzi wa kampuni ya uuzaji wa magari ya FG Trucks & Equipments Ltd , Hamis Hassan amesema Mwanzo wateja walikua hawaamini kama magari hayo yatakuwa na ubora sawa lakini kwa kipindi hiki magari yapo mitaani na yanafanya vizuri kinyume na matarajio.

Aidha Kiwanda hicho kilichopo Kibaha Mkoani Pwani tayari kimeajiri Wafanyakazi 100 ambao wana ajira za kudumu na wengine wana ajira za mkataba.