Na Mwandishi Wetu,Timesmajira online
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini ameagiza kukamilika kwa wakati mradi wa ujenzi wa kituo cha Polisi Daraja B cha Wilaya ya Butiama mkoani Mara, ifikapo Desemba 2023 kama ilivyoelekezwa.
Maagizo hayo ameyatoa Novemba 18, 2023 wakati alipofanya ziara ya kutembelea na kukagua uendelezaji wa mradi wa ujenzi wa kituo hicho kilichopo katika eneo la Mtuzu Kata ya Butiama Wilayani Butiama.
“Nimefurahishwa na kasi ya mradi wa huu unatekelezwa na serikali bila kuchoka mama huyu(Rais Samia)amemwaga fedha za kutosha hivyo basi nimtake mkandarasi kukamilisha mradi haraka bila vikwazo kwani wananchi wana kiu kubwa ya kupata huduma karibu,”amesema.
Katika taarifa yake Meneja wa mradi huo wa Kikosi cha Polisi Ujenzi, Mkandarasi SP Masiva Mfinanga ameeleza kuwa mradi huo una thamani ya Milioni 802 ambao ulianza rasmi Mei 6, 2023 na unategemewa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba 2023.
Hata hivyo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi na Mbunge wa Jimbo la Butiama Jumanne Sagini yupo mkoani Mara kwa ziara yake ya kikazi ambapo atatembelea na kukagua miradi mbalimbali ya ujenzi inayoendelea katika Vyombo vya Ulinzi na Usalama vilivyopo chini ya Wizara hiyo.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best