Na Esther Macha,Timesmajira Online, Masasi
IMEELEZWA kuwa kukamilika kwa kituo cha afya Mtandi katika Mji Masasi mkoani Mtwara kutapunguza msongamano wa wagonjwa katika hospitali ya Mkomaindo .
Kitendo cha kukamilika kwa kituo hicho afya kitaleta neema na kitakuwa tegemeo kubwa kwa wananchi wanaokizunguka kituo hicho ambapo serikali ilitoa jumla ya shilingi mil.500 ili kituo hicho kiweze kukamilika.
Akizungumza leo wakati wa ziara yake kutembelea miradi ya Maendeleo , Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Mji Masasi ,Erica Yegella amesema kuwa tayari majengo ya kituo hicho yamekamilika na kimeanza kutoa huduma ikiwemo maabara ,duka la dawa na sehemu ya kupokelea wagonjwa.
“Kituo chetu sasa kinaenda kufunguliwa rasmi ili kupunguza msongameno katika hospitali yetu kubwa ya Mkomaindo ambayo ni hospitali ya siku nyingi,lakini kituo chetu cha Mtandi ni kikubwa na tunashukuru sana serikali katika kuboresha afya sisi kama halmashauri ya Mji tunajivunia kuwa na kituo hiki sababu ni kituo cha mfano na halmashauri yetu tuna kituo cha kimoja Cha afya na hospitali moja”amesema Mkurugenzi huyo.
Kaimu Mganga Mkuu kituo cha afya Mtandi ,Dkt.Nelson Kimaro amesema kuwa kituo hicho kimejengwa kwa mil.500 ambapo fedha hizo na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Samia Suluhu Hassan.
“Pia kituo kimekabidhiwa vifaa tiba vyenye thamani ya mil.150 lengo likiwa ni kukiwezesha kituo hicho cha afya kuweza kuhudumia wananchi kwa ufasaha wananchi wafike kupata tiba hata wanaotoka wilaya za jirani na maeneo yote yanayozunguka kituo hivi sasa kuna vifaa vya kisasa vya kutosha “amesema Dkt.Kimaro.
Mwanahawa Abdi Said ni Mtaalam wa Mabaara kituo cha afya Mtandi amesema kuwa kituo hicho kimenufaika kwenye vifaa tiba ambapo wana mashine ya kupima figo na ini ,tunapoletewa mashine yeyote tuna uwezo wa kupima sababu tumesoma.
More Stories
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa