December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kisarawe Ushoroba Festival kufanyika tena mwaka 2022

Na David John,Timesmajira,Online

HALMASHAURI ya Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani imeweka wazi baada ya kufanikiwa kwa tamasha la Kisarawe Ushoroba Festival mwaka 2021, imesema kwamba Kisarawe Ushoroba Festival 2022 litafanyika ndani ya wilaya hiyo na wadau wameridhia kwa kauli moja.

Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe  Jocate Mwegelo ameweka wazi wilaya yao imejipanga kuendelea na Kisarawe Ushoroba Festival na kwa mikakati iliyopo wana uhakika mwaka 2022 kutakuwa na mambo mengi zaidi ukilinganisha na Kisarawe Ushoroba Festival 2021.

Aidha ameanza kukaribisha wadau na kuwashukuru WWF Tanzania na Vodacom Tanzania Foundation ambao wameahidi kuendelea kudhamini tamasha hilo.