Na Judith Ferdinand, TimesMajira Online, Mwanza
Kupitia fedha za Uviko-19,Wilaya ya Ilemela imefanikiwa kutekeleza miradi ambayo imezinduliwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa kwa mwaka 2022 Sahili Geraruma.
Ambapo miongoni mwa Miradi iliyozinduliwa ni pamoja na mradi wa maji katika eneo la mlima wa Rada ulioponkata ya Kiseke wenye thamani ya milioni 365.5(365,580,080.00).
Akizindua mradi huo Geraruma amewataka wanufaika kuhakikisha wanatunza miundombinu yake kwa manufaa yao na vizazi vijavyo.
Mradi huo umefadhiliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19.
Hata hivyo mradi huo utasaidia kupatikana kwa huduma za maji ndani ya Kata ya Kiseke hususan kwa wakazi wa eneo la mlima wa Rada ambapo utanufaisha jumla ya wakazi 3,600 hivyo kuongeza kiwango cha upatikanaji wa majisafi na salama kwa wakazi wa maeneo husika.
Mbali na mradi huo pia Kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa Sahili Geraruma amezindua mradi wa ujenzi wa madarasa 4 katika shule ya Bujingwa uliopo Kata ya Buswelu Wilayani Ilemela yaliyogharimu kiasi cha Milioni 80.
Fedha za mradi huo zimetoka Serikali Kuu kupitia mpango wa maendeleo kwa ustawi wa Taifa na mapambano dhidi ya UVIKO-19 ambapo ameagiza uongozi wa shule kuhakikisha maelekezo yaliyotolewa yanafanyiwa kazi ili wanafunzi wasome katika mazingira bora.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa