Na Mwandishi wetu, Dar es Salaam
KATIKA kuadhimisha sikukuu ya Mapinduzi Zanzibar, waandaaji wa mashindano ya binti Afrika, Hotel ya Kingazi iliyopo Mbagala Kijichi jijini Dar es Salaam, inawatakia heri Watanzania wote katika maadhimisho haya.
Akitoa harii hizo leo, Mkurugenzi wa Hotel ya Kingazi, Nelson Mahenge amesema heri hiyo pia imuendee Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kwenye
maadhimisho ya miaka 60 ya mapinduzi Zanzibar.
Amesema, anawapongeza marais hao kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuiongoza nchi na kuijenga.
Amewataka Watanzania wote kuunga mkono juhudi kubwa zinazofanywa na marais hao ili mafanikio nakubwa zaidi yaweze kupatikana.
“Sisi kama Hatel ya Kingazi ambao ndio waandaaji wa mashindano ya urembo ya binti Afrika, tunawatakia heri ya sikukuu katika kuadhimisha miaka 60 ya Mapinduzi Zanzibar.
“Lakini pia, tunaunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kutokana juhudi kubwa wanazozifanya katika kuijenga nchi,” amesea Mahenge.
Hotel ya Kingazi iliyopo Mbagala Kijichi ndio waandaaji wakubwa wa mashindani ya binti Afrika, lakini pia wallimbwende hao ndipo watakapopiga kambi ya miezi minne kabla shindano hilo kuanza.
Hata hivyo Mkurugenzi wa hotel hiyo, Nelson Mahenge amesema wamejipanga vizuri kwa ajili ya kupokea wageni kutoka nchi mbalimbali za Afrika, huku akiahidi kutoa huduma bora pamoja na usalama wa kutosha.
Mbali na hivyo, hotel hiyo hutoa huduma mbalimbali ikiwemo malazi, chakula na vinywaji vya aina mbalimbali, washiriki wanatakiwa kujisikia huru pindi watakapopiga kambi katika hotel hiyo.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua