Na Penina Malundo,Timesmajira
RAIS Mstaafu awamu ya nne, Jakaya Kikwete, amesema kwa sasa Afrika inazidi kusonga mbele na mafanikio kuanza kuonekana ikiwemo uchumi wa Nchi za kiafrika kuzidi kuimarika na kuwa imara.
Pia amesema maisha ya Mamilioni ya wananchi wa Afrika yameimarika na kupungua kwa umasikini kiuchumi,kuimarika kwa afya,elimu na vijana kuwezeshwa.
Ameyasema hayo leo Kampala ,Uganda katika Kongamano la nane la Kikanda la Viongozi Afrika (ALF)lililoanza jana na kumalizia Aprili 8 mwaka huu lililoandaliwa na Taasisi ya Uongozi ambapo Kikwete ndio Mlezi na Mratibu Mwenza wa Jukwaa la hilo,alisema ni ukweli ni kwamba Afrika iliyopo leo siyo Ile ambayo ilirithiwa kabla ya uhuru.

Amesema hata kama wanasherekea mafanikio yao wanatakiwa kuwa macho juu ya changamoto zinazolikabili bara la Afrika ambayo ni umasikini,maradhi,kutokua na usawa na mabadiliko ya tabia ya Nchi.
“Miaka ya hivi karibuni tunaweza kushudia namna Afrika inasonga mbele, na mafanikio yetu ya kiuchumi .
“Hata tunaposherehekea mafanikio yetu, lazima tukumbuke changamoto zinazoendelea ambazo zinatishia maendeleo yetu-umaskini, magonjwa, ukosefu wa usawa, kutojua kusoma na kuandika, na mabadiliko ya hali ya hewa yanasalia kuwa wasiwasi,”amesema Kikwete
Amesema ni vema kama viongozi wa Afrika kuwa na dhamira yao thabiti ya kutumia teknolojia na uvumbuzi ili kuleta mabadiliko katika kufikia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ifikapo 2030.
Amesisitiza kuwepo kwa uharaka wa pamoja katika kuchukua hatua ya kwenda na mbinu za biashara na kukumbatia mageuzi muhimu na kwa ujasiri ambapo yanahitaji uhamasishaji wa rasilimali, utashi thabiti wa kisiasa, na kuimarishwa kwa uwajibikaji.
“Jukwaa hili limekua na mijadala yakujenga juu ya changamoto na fursa na mienendo ya ulimwengu inayoathiri maendeleo ya bara la Afrika.
“Kila mwaka jukwaa hili linakua na mada ya kimkakati ambapo mada ya kikao cha Saba mjini Accra Ghana iligusia,mabadiliko ya kiuchumi,ushirikiano,ulinzi na amani,usimamizi wa maliasili ili kukuza biashara ya kilimo baina cha kikanda,”amesema Kikwete

Amesema mwaka huu jukwaa hilo linaongozwa na mada kuu ambayo ni Kutambua maendeleo endelevu ,malengo katika maendeleo ya Afrika na namna yakusonga mbele.”Ndani ya Jukwaa hili tutajadili mambo manne ni pamoja na kukagua hali ya sasa ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Afrika (SDGs) ,kubaini changamoto zinazozuia Maendeleo ya Kikanda ,Kukuza ushirikiano wa kikanda na kubadilishana maarifa miongoni mwa Nchi za Afrika pamoja na kuvumbua suluhisho la mambo na ushirikiano wa kimkakati kwaajili ya kuharakisha maendeleo.
Amesema mada iliyochaguliwa itawapatia fursa tofauti siyo tu kufurahia maendeleo ya Afrika bali pia kuhakisi vikwazo vya ndani kabisa katika bara la Afrika.

Naye Rais wa Mstaafu wa Sierra Leone Dkt. Ernest Bai Koroma amesema Afrika inahitaji kupata teknolojia, fedha, biashara ya haki, na fursa katika kuungwa mkono na wananchi wa nchi hizo.
“Jukwaa hili liwe zaidi ya mazungumzo tu,bali liwe ni hatua ya mabadiliko na wakati ambapo tunajitolea kujenga Afrika ambayo ni bora ,” amesema.
Ametoa wito kwa viongozi hao kuimarisha kwa ushirikiano wa ufanisi, kuvunja migawanyiko, na kuwekeza kwa watu kama vile walimu, wauguzi, wabunifu na wajasiriamali.
More Stories
Boshe:ALF imekutana kutambua Maendeleo Endelevu ya Bara la afrika
Diwani awapa bima za afya watoto wa mahitaji maalum
Rais Mwinyi:Tuzindue mpango wa ujuzi kwa vijana katika uchumi wa buluu