May 17, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kikwete awataka wahadhiri kutafuta sababu wanafunzi kufeli Hesabu, Sayansi

Na Iddy Lugendo, Timesmajira Online DSM

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amewataka wahadhiri kutafuta sababu ya ongezeko la idadi ya wanaofeli somo la hesabu na sayansi ili kujua udhaifu kwa sababu kama wanafunzi hawafanyi vizuri kwenye masomo hayo safari ya maendeleo nchini itachelewa.

RAIS Mstaafu Dkt. Kikwete ametoa kauli hiyo Agosti 31,2023 jijini Dar es Salaam muda mfupi baada ya Wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara kuahidi kuchangia jumla ya sh bilioni 465 kwa ajili kuiwezesha serikali kupata kiasi cha Dola za Marekani milioni 50.

“Mmetoa ahadi, ahadi ni deni, Singida mmeahidi sh milioni 88, Mtanda (Mkuu wa Mkoa wa Mara) mmeahidi sh milioni 100 heee! mtoe jamani, msitoe ahadi kama za Fund raising.” Amesema Kikwete na kuongeza

“Jumla ya milioni 465, nawashukuru sana ila msinitie aibu, msiniaibishe ahadi ziwe kama za Fundraising watu wanajitokeza ili tu wapate kupiga picha na Rais akaitumie kwenye mambo yake utasikia mtu wangu sana huyu, picha na Rais unaenda kuombea mkopo benki. ” Amesema Kikwete na kufanya wahudhuriaji kuangua vicheko.

Akisisitiza anasema “Mimi ndio Mwenyekiti wa GPE Dunia, napeleka ripoti tumefanya mkutano mkubwa wa Wadau tumekusanya kiasi hiki, sasa sio upite mwezi wa tisa, wakumi, wakumi na moja holaa! Desemba wanakuja;……

“Sitaki wakifika waniulize mchango wa wadau sekta ya elimu upo wapi, mtaniaibisha, mtanidhalilisha sana, nitajitahidi kusema tupo kwenye mchakato, lugha ya Watanzania, Mzee mambo yanakwenda usiwe na wasiwasi. ” Anasema Kikwete na kuangua kicheko.

Katika hafla hiyo, Mkoa wa Mara umeahidi kutoa sh Milioni 155, Singida sh bilioni 88, Tanga sh bilioni 14, Njombe sh bilioni 7.8, Lindi sh bilioni 4, Shinyanga sh bilioni 5.7, Pwani sh bilioni 55.8 na Songwe sh bilioni 9.

Mikoa mengine ni Kagera imeahidi kutoa sh bilioni 6.3, Simiyu sh bilioni 6.5, Manyara sh bilioni 13.7, Geita sh Bilioni 11.4 , Arusha sh bilioni 8.3, Dodoma sh bilioni 14.5, Iringa sh bilioni 5, Mtwara sh bilioni 6.2 Katavi sh 24.9, Kilimanjaro sh bilioni 6.7, Mbeya sh bilioni 4, Kigoma sh 5.2, Dar es Salaam sh bilioni 20, Rukwa sh bilioni 4.1, Morogoro sh bilioni 16.25, Mwanza bilioni 9.4 na Ruvuma sh bilioni 4.9.