Na Penina Malundo, timesmajira
NAIBU Waziri wa Uchukuzi, David Kihenzile
ameitaka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA) kuhakikisha wanasimamia miradi yao kwa kuangalia muda uliopangwa ili iweze kukamilika kwa wakati na kuanza kufanya kazi.
Ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam,Naibu Waziri huyo alipotembelea ofisi za Mamlaka hiyo alisema lengo kubwa kwenye ziara ya TCAA ni kufahamiana na kupata fursa ya kuonana na Menejimenti kuona wanafanya nini na wana mipango gani ambayo watayapa kipaumbele.
Amesema wanapaswa kuendelea kusimamia ubora wa miradi hiyo na thamani ya fedha wanazotoa zinatakiwa kuwekewa utaratibu mzuri wa kusimamia maelekezo yaliyotolewa na viongozi yawe na mfumo ya utekelezaji.
“Zaidi ya mabilioni yameelekweza na bado Rais Dk. Samia Suluhu Hassan anatenga fedha ili kuhakikisha usalama wa vifaa vya mbalimbali vya angani ambavyo kimsingi vina dhibitiwa na vina simamiwa na TCAA,”amesema.
Aidha amesema ipo miradi kadhaa ambayo inafanyika mikubwa mojawapo ni ujenzi wa chuo cha usafiri wa anga ambacho kinafanya kazi kufundisha watu mbalimbali.
Kihenzile ametoa wito ndani na nje viwanja vya ndege usafiri wa anga nchini ni salama kuliko mahali popote kwa sasa, hivyo mashirika, wawekezaji , wafanyabiashara waingie kwenye usafiri wa anga kuwekeza kwa kuwa kupo salama.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Anga (TCAA),Hamza Johari amesema lengo la Waziri kuja katika mamlaka hiyo ni kufahamu Mamlaka hiyo na majukum wanayofanya ambapo ameridhishwa na kazi ambazo wanafanya.
“Naibu Waziri waametoa maelekezo ikiwemo katika suala zima la miradi kuhakikisha kwamba wanafanya miradi hiyo kwa viwango na ubora unatakiwa na inamalizika kwa wakati,” amesema Johari.
Amesema mradi wa kubadilisha mifumo ya sauti ambayo wanaendelea nayo , kuboresha mawasiliano na mradi wa ujenzi wa chuo cha usafiri wa anga.
Amesema katika miradi hiyo yote mitatu watahakikisha maelekezo yatafanyiwa kazi kuwa miradi inafanyika kwa ubora na kumalizika kwa wakati kuwa viwango vya kimataifa.
More Stories
Tanzania kuwa mwenyeji Mkutano wa Kimataifa matumizi bora ya Nishati
Madiwani Ilala watoa chakula kwa watoto yatima
Waziri Mkuu: Tumieni matokeo ya tafiti za kisayansi katika utekelezaji wa mipango ya kitaifa