February 28, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Khimji kumchangia Zungu fomu ya Ubunge

Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Ilala

DIWANI wa Kata ya Ilala Saady Khimji,amesema atamlipia gharama za fomu kwa nafasi ya Ubunge katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025,Mbunge wa sasa wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu.

Kimji ,amesema hayo wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi(CCM),ambapo ameeleza sababu ya kufanya hivyo ni kuwa Ilala bado inamhitaji Mbunge huyo.

Amesema awali alikabidhi kiasi cha milioni 1,kwa ajili ya kumchangia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan, kugombea Urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huu.