Na Esther Macha, Mbeya
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imeahirisha kesi ya usafirishaji wa dawa za kulevya gramu 23.4 inayomkabili kada wa CHADEMA, Mdude Nyagali baada ya mawakili wa upande wa utetezi kutohudhuuria mahakamani.
Awali imeelezwa mahakamani hapo leo na Wakili Mwanadamizi wa Serikali, Lugano Mwakilasa kuwa mawakili wa upande wa utetezi Mei 27, ilipotajwa kesi hiyo waliandika barua ya kuomba rufaa ambayo iliwasilishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kufanyiwa maamuzi.
Wakili Mwakilasa amedai kwa sasa kinachosubiriwa ni majibu ya rufaa hiyo ili kesi iendelee kusikilizwa tena na kuhusu mawakili hao kutofika mahakamani, alidai hawana taarifa zao.
Kufuatia maelezo hayo hakimu amemtaka mtuhunmiwa kuwasiliana na ndugu zake ili waweze kuwasiliana na mawakili wanaomtetea kujua sababu za kushindwa kufika mahakamani na kwamba ni wajibu wao kuhudhuria kusikiliza kesi hiyo.
Baada ya hapo shauri hilo limeahirishwa hadi Juni 17, mwaka huu litakapotajwa tena na mtuhumiwa amerudishwa rumande.
More Stories
Amos Lengael Nnko afariki kwa ajali ya gari
Gridi za Tanzania, Kenya kuimarisha upatikanaji wa umeme
Mama Zainab:Watoto yatima ni jukumu la jamii yote