January 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kesi 41 za COVID-19 zagundulika Copa America

BRASILIA, Brazil

WIZARA ya afya nchini Brazil imesema, Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Amerika Kusini yajulikanayo (Copa America), yamekumbwa na visa 41 vya COVID-19 baada ya wachezaji 31 ​​na wafanyakazi 10 wanaoshiriki katika mashindano hayo kukumbwa na virusi vya ugonjwa huo.

Taarifa hiyo imesema, wafanyakazi wote waliotambuliwa kuwa na virusi walikuwa Brasilia, ambapo Brazil ilianza mashindano hayo mwishoni mwa wiki kwa ushindi wa goli 3-0 dhidi ya Venezuela. Hata hivyo, Kikosi cha wageni cha Venezuela kilikuwa kimepungua kutokana na kesi 12 za COVID-19 zinazohusu wachezaji na wafanyakazi.

Rais wa Brazil Jair Bolsonaro alijitolea kufanya mashindano hayo nchini humo wiki mbili tu zilizopita baada ya Argentina na Colombia kupigwa chini uwenyeji wa mashindano hayo. Yeye ni mkosoaji wa sera za kutenganisha kijamii na anasema athari za kiuchumi zinaua zaidi ya virusi.

Mmoja wa makocha wa mazoezi ya mwili wa timu ya Taifa ya Peru alipima na kugundulika kuwa na virusi vya COVID-19 huko Lima. Hivyo hatasafiri kwenda Brazil. Haikufahamika ikiwa alihesabiwa na wizara ya afya ya Brazil kama moja ya kesi zilizothibitishwa zinazohusiana na mashindano hayo.

Colombia nayo imesema, msaidizi wake wa kiufundi Pablo Roman na mtaalam wa viungo Carlos Entrena wana virusi hivyo vya Corona.Venezuela ilitangaza kuwa imeita wachezaji 15 wapya wa kikosi hicho kwa taarifa fupi baada ya wanane kupimwa wakiwa na Corona baada ya kuwasili nchini Brazil.