Na Heri Shaaban, Timesmajira Online,Dar
MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar-es-Salaam Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa Kata ya Vingunguti,amesema anaweka matenki makubwa ya maji kwenye Kata hiyo ili kumtua ndoo mama kichwani na kutatua kero ya maji.
Kumbilamoto amesema hayo katika kikao cha kuelezea mikakati ya maendeleo na kutatua kero huku akisema kipaumbele chake ni kusambaza maji ili kumtua ndoo mama kichwani.

Amesema upo mpango wa muda mfupi kwa kushirikiana na DAWASA wataleta matanki makubwa ya maji safi ambayo yatasambazwa kila mtaa huku wakisubili mpango mikubwa wa kufufua visima pamoja na wa kuunganishwa kwenye mfumo mikubwa wa maji ya Ruvu.
Pia amesema kwa muda mrefu Vingunguti wamekuwa wakinunua ndoo moja ya maji safi na salama kwa shilingi 1000 kupitia mpango huo watanunua ndoo moja kwa shilingi 100 .
Kwa upande wake Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata Mhandisi Gilbert Masawe,amesema hatua hiyo ni ya dharura lakini kuna mpango mkubwa upo hatua ya awali ya utekelezaji ikiwemo kufufua visima vyote vilivyotelekezwa.

Pia kuangalia namna ya kusambaza maji kupitia mradi mkubwa wa Ruvu ambao kwa kiasi kikubwa unatumiwa na wakazi wa Mkoa wa Dar-es-Salaam.
“Tunavyo visima vyetu humu, tutavifanyia tathimini ili tujue vinahitaji nini ili tuviboreshe viweze kufanya kazi,lazima tujihakikishie usalama wa maji na kiasi gani kipo,”amesema Masawe.

More Stories
The Desk and Chair yatoa vifaa saidizi kwa Masatu na mkewe
jengo la mama,mtoto la bilioni 6.5 lazinduliwa Mbulu
Dkt.Malasusa ataka hospitali ya Haydom kuombea wafadhili wanaoishika mkono