December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kelvin aibuka kidedea nafasi ya uwenyekiti UVCCM Ruvuma

Na Mwandishi wetu,Timesmajira

Kelvin Kelvin Challe ameshinda nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Chama cha Mapinduzi (Uvccm) Mkoa wa Ruvuma baada ya kupata kura 266 kati ya 490 zilizopigwa na wajumbe.

Akitangaza matokeo hayo jana ,Msimamizi wa uchaguzi huo,Juma Nambaila ambaye ni Katibu wa Chama cha Mapinduzi Songea Vijijini ,alimtangaza Adamu Dominicus Nyanguru amepata kuravl 13,John Foroteo Haule kura 198,Kelvin Kelvin Challe kura 266 na Jummy Juma Pandu kura 10.

Nafasi ya Ujumbe Baraza Kuu Uvccm Taifa,aliyeshinda Frank Francis Muhuwa kwa kura 258,Jordan Renatus Shawa na Msyang Men Kuruchumila kura 195.

Kwa upande wa Uvccm kwenda UWTHallanes Mwabalogile amepata kura 18,Happines Julius Nganena kura 198 na Irene Lucas kunambi kura 248.

Aidha kwa nafasi ya Uvccm kwenda Wazazi mgombea Geredia Daimon Hamuya amepata kura 74 na Sikuzan Rashid Rai amepata kura 87.

Kwa upande wa Mkutano Mkuu Uvccm Taifa mgombea Eva Castory alipata kura 176,Geredia Hamuya kura 25 na Mercy Ngatunga kura 261.