Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
BENKI ya KCB nchini, imedhamini mbio za Mount Meru Marathon zitakazofanyika jijini Arusha mwakani zikiwa na lengo la kumuinua mtoto wa kiume aweze kurejea kwenye nafasi yake.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa Mount Meru Marathon Desemba 9, mwaka huu, kwenye Bonanza lililofanyika katika viwanja vya Ngarenaro Arusha, Meneja wa KCB Benki tawi la Arusha TFA, Hogla Laizer alisema wapo kwa ajili ya kudhamini mbio hizo.
Hogla alisema, KCB Benki imekuwa mstari wa mbele katika kudhamimini michezo mbalimbali, licha ya kutoa huduma za kifedha kwa sababu wadau wa michezo wamekuwa wengi.
“Tumekuwa tukifadhiri michezo mbalimbali na tukidhamini matukio ambayo yanalenga kuinua vijana kwa sabau tunaamini michezo ni ajira ambayo inamuwezesha kijana kupata kipato
Hata hivyo alisema, wamevutiwa na Mount Meru Marathon kwa sababu ni matukio ambayo yanalenga vijana kwenye michezo.
Aidha, alisema wao kama KCB Benki mbali ya kutoa huduma za kifedha lakini ni wadau wakubwa wa michezo.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mount Meru Marathon, Bernadinnah Senen Mosha alisema
mbio hizo ni za muda mrefu sana kwa wakazi wa Arusha, na sasa zimekuja kivingine.
“Namshukuru mwenyezi Mungu kwa kufikia leo Desemba 9, 2023 kufikia kilele cha kuzindua mbio za Mount Meru Marathon, tumeweza kushirikisha vijana wengi wazee na watoto.
“Dhana kubwa ya mbio hizi tunahakikisha inarudisha heshima kwa wana Arusha katika suala zima la michezo, Mbio za Mount Meru Marathon zikiwepo kwa miaka mingi sana kabla Kill Marathon, lakini tuliweza kwenda na kupokea kijiti.
“Lengo kubwa la Mount Meru Marathon Sports Club Foundation Promotion ni kuhakikisha tunawasaidia Wazee, walemavu, watoto wote na watoto wote wa mitaani wanaoishi katika mazingira magumu.
Bernadinnah alisema, bila ya kukuza kizazicha sasa na kuwaangalia wakiwa wakubwa watakuwa wameharibu kizazi kwa hiyo lazima wawatengezee mazingira mazuri bila ya kutumia njia ya mkato.
“Tuna mikakati ya kuwaendeleza vijana ambao wanahitaji kujikwamua na kufikia malengo yao, Maount Meru Marathon imeanzisha Program kwa vijana kwa ajili ya kuwawezesha kuingia katika kilimo, ufugaji, ujasiriamali pamoja na biashara.
“Course hizo tutatoa bure na baada ya kuhitumu miezi mitatu zitawawezesha vijana kuanza biashara ndogondogo na baadaye kufikia kwenye biashara kubwa, hiyo ndio azma yetu kubwa.
“Natamani kila Mwananchi hasa mwana Arusha awe mwakilishi mkubwa hasa mtoto wa kiume, lakini tunatakiwa kutoa haki za msingi kwa walemavu, kwa hiyo Mount Meru itawapatia jezi na mipitra walemavu wote ambao wameshiriki mechi za leo.
“Na yote ni juhudi kubwa ya kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungao wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, hili Taifa haliwezi kujengwa bila ya sisi wenyewe.
Aidha, aliishukuru Serikali kwa kuwawezesha mpaka kufika Desemba 9, 2023, kwa ajili uzinduzi wa Mount Meru Marathon, pia alimshukuru mwenyekiti wa CCM Arusha, kwa kutoa ushirikiano wa hali ya juu kwenye uzinduzi huo pamoja na vyombo vya habari pi vyombo vya usalama.
Pia aliiomba serikali kwa ajili ya kufufua milango ya kupata fursa lakini alivitaka vyama vingine viunge mkono katika jitihada hizo za kumkwamua mtoto wa kiume.Bila kusahau vilabu vingi vya mbio na vyama vya joging.
Alisema, Mount Meru Mrathoni kutakuwa na mbio kilometa 21, 10,5 na mbili na nusu, mashjindano ya Baiskeli na pia wapanda mlima dhana kubwa ni ‘Mtoto wa kiume arudi kwenye nafasi yake’.
Naye mmoja wa waliondaa mbio za Mount Meru Marathon, Patricia Patrick alisema wamezindua mbio za Maount Meru Marathon ili kumkomboa mtoto wa kiume aweze kujiamini katika jamii.
“Tunashukuru sana Tanzania na Rais wetu Dkt. Samia Suuhu hassan kwa kutupa kipaumbele vijana hasa kupitia michezo kuwafanya vijana kupata kipato kupitia tasnia hiyo.
“Nawahamasisha vijana wenzangu wapende michezo kama njia mbadala ya kuepekana na dawa za kulevya lakini pia magonjwa yasioambukiza.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania