March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kazukamwe aahidi kuipa thamani ardhi jimboni Nkasi Kaskazini

‎Na Israel Mwaisaka,Timesmajira Online-Nkasi

‎Mgombea Ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)  Jimbo la Nkasi Kaskazini,Salum Kazukamwe  amewataka Wananchi kutunza rasilimali ardhi waliyonayo na kuachana na fikra ya kuiuza.

Ambapo amesema,kuiuza hakuto wawezesha kukabiliana na umaskini na badala yake watumie kuanzisha shughuli mbalimbali za uwekezaji.

‎Kazukamwe,amesema hayo katika mkutano wake wa kampeni vijiji vya Mkole na Ipanda Kata ya Nkomolo,ambapo amedai kuwa ardhi ni moja ya rasilimali muhimu katika kuyafikia maendeleo,hivyo ufike wakati waachane na mawazo hafifu ya kuiuza bali waitumie kuweza na kujiendeleza kimaisha.

‎Amesema kuwa kama atapata ridhaa ya kuchaguliwa kuwa Mbunge moja kati ya mambo atakayoyafanya ni kuipa ardhi thamani ili wale waliyonayo waweze kunufaika nayo.

‎Pia amesema atashughulikia changamoto ya ukosefu wa maji na ujenzi wa zahanati nzuri katika vijiji hivyo.


‎Kwa upande wake gombea Udiwani wa kata ya Nkomolo,Stephen Tontololo, amesema Kata hiyo ‎ inakabiliwa na changamoto nyingi ambazo zinahitaji Diwani makini ambaye ni yeye, ataweza kuzishirikisha changamoto hizo kwa wadau wengine wa maendeleo ikiwemo serikali ili kuzitatua.

‎Katibu wa CCM wa Wilaya ya Nkasi Anastasia Almasi,amewasisitiza wananchi kuchagua mafiga matatu kwa maana ya Rais,Wabunge na Madiwani wote watokanao na chama hicho.