Na Mwandishi wetu Timesmajira online
CHAMA Cha Wamachinga Kariakoo (KAWASO) kimesema hadi kufikia sasa jumla ya wafanyabiashara wadogo wadogo 560 waliokuwa wahanga wa jangaa moto lililotokea hivi karibuni katika soko la Kariakoo wameshapatiwa maeneo ya kufanyia biashara pamoja na meza.
Hayo yamesemwa mkoani Dar es salaam hivi karibuni na Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Namoto Namoto wakati akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema KAWASO imetenga minne kwa ajili ya kuwahamisha wahanga hao katika mtaa wa Swahili 346, Sikukuu 342 na bado inaendelea kuagiza meza zingine zitakazopangwa katika mtaa wa Kongo na Manyema.
Amesema wahanga wote ni zaidi 7,000 na KAWASO inatarajia kutoa meza kwa wahanga wote na kuwataka wafanyabiashara wadogo wadogo ambao ni wahanga kuwa na subira.
“Serikali ilitoa maelekezo kwetu ya kuwahamisha baadhi ya wafanyabiashara wadogo wadogo waliokuwa wakifanya biashara zao katika maeneo ya Tandamti, Nyamwezi, Swahili na Mtaa wa Mkunguni, sisi kama Taasisi tayari tumetoa meza 560 kwa wahanga,” Namoto.
Amesema kabla ya kutoa meza hizo KAWISO ilitoa elimu katika baadhi ya maeneo ambayo tayari kulikuwa na wafanyabiashara wadogo wadogo ili kuondoa sitofahamu baina yao.
Katika hatua nyingine, Namoto ameziomba Mamlaka za Serikali zinazohusika na masuala ya biashara kushirikiana kwa pamoja na wafanyabiashara wadogo ili kutatua changamoto zinazowakabili.
Amesema Mamlaka za hizo hazina ofisi maeneo ya soko hilo hali ambayo inachangia wamachinga wengi kutokuwa na elimu juu ya namna ya taasisi hizo zinavyofanya kazi.
Amezitaja baadhi ya Mamlaka hizo kuwa Ni pamoja na Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Ushindani Tanzania(FCC), Wakala wa usajili Biashara na Leseni (BRELA) pamoja na maofisa wa biashara.
Amesema mamlaka hizo zingekuwepo karibu zingesaidia kutoa elimu kwa ukaribu kwa Wafanyabiashara.
” Hapa kariakoo kuna wafanyabiashara mbalimbali wachache ndio wanajua kazi za Taasisi hizo, hivyo uwepo wa taasisi hizi katika eneo hili kutasaidia sana wafanyabiashara wadogo kuwa na uwelewa wakutosha wa namna ya taasisi hizo zinavyofanya kazi,” amesema Namoto.
Aidha amewaomba wafanyabiashara wadogo kujitokeza kuchukua vitambulisho vya ujasiliamari ili waweze kupata fursa mbalimbali ikiwemo mikopo ya Biashara kutoka Taasisi za fedha, kwani vitambulisho hivyo vimekidhi vigezo vya kupata mikopo hiyo.
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi