Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online SAME
KATIBU Tawala wilaya ya Same Upendo Wella amewaomba watumishi na wadau mbalimbali wilayani humo kumpa ushirikiano ili kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake na kumsaidia Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassani katika kuijenga nchi.
Upendo ameyasema hayo wakati akikabidhiwa ofisi na katibu tawala alihamishwa Sospeter Magonera ambaye amehamia wilaya ya Hai.
Amesema ili maendeleo yaweze kupatikana lazima kuwe na ushirikiano wa kutosha katika kazi ambapo amewasisitizia Watumishi kuwa na umoja, upendo miongoni mwao.
“Kazi yetu kubwa ni kuwahudumia wananchi wa Same kwa kusimamia vema utekelezaji wa miradi mbalimbali na kutatua migogoro inapotokea katika wilaya yetu “amesema Upendo
More Stories
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba
TRA kuongeza idadi ya waendesha uchumi walioidhinishwa
TRA Tanga wajivunia ukusanyaji mapato