Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katibu Mkuu Msaidizi na Mratibu Mkuu wa Kimataifa wa mapambano dhidi ya UVIKO-19 kutoka Shirika la Afya duniani (WHO) Dkt. Ted Chaiban anatarajia kuja nchini Tanzania mwanzoni mwa mwezi Julai 2022
Akizungumza na Waziri wa Afya Mwakilishi Mkazi wa WHO nchini Tanzania Dkt.Zabulon Yoti amesema kuwa Kiongozi huyo anatarajia kuwasili nchini kwa ziara ya siku nne kuanzia tarehe 4 hadi 7 mwezi ujao ambapo atapata nafasi ya kutembekea Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Dodoma
Amesema lengo la ziara hiyo hapa nchini ni kuhamasisha wananchi kupata chanjo ya UVIKO-19 pamoja na masuala mengine ya Afya.
Wizara ya Afya hivi karibuni ilizindua kampeni ya Global Vax Initiatives yenye lengo la kuhamasisha jamii kupata chanjo ya UVIKO-19 pamoja na kufuatilia wale ambao hawakukamilisha chanjo zenye dozi mbili.
More Stories
Serikali kuwezesha CBE kuwa kituo mahiri
TCC yaibuka kidedea tuzo za PMAYA
Mwanafunzi apoteza maisha kwa kushambuliwa na mamba