January 11, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu Mkuu Maliasili na Utalii ahimiza bidii na ushirikiano kwa watumishi

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Francis Michael amewataka watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wafanye kazi kwa bidii huku akisisitiza kuwa yeye kama kiongozi wao ataendelea kuwapa ushirikiano mkubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

Ameyasema hayo leo jijini Dodoma mara baada ya kuwatembelea watumishi hao katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii zilizoko katika Chuo Kikuu cha Dodoma na kuwahakikishia kuendelea kuwapa ushirikiano mkubwa ili waweze kutimiza majukumu yao ya kila siku.