Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge) Dkt. John Jingu amepongeza maendeleo ya utekelezaji wa zoezi la Anwani za Makazi Jijini Mbeya wakati alipokutana na Kamati ya utekelezaji wa zoezi hilo mkoani humo.
Ametoa pongezi hizo wakati alipotembelea na kukagua utekelezaji wa anwani za makazi wakati wa ziara yake ya siku tatu kuanzia tarehe 16 hadi 18 Mei, 2022 mkoani humo.
Aidha alikagua shughuli za uchakataji wa vibao vya nyumba pamoja na nguzo za barabara na mbawa zake vinavyotengenezwa katika karakana ya Allyrich iliyopo eneo la Soweto alielekeza kuongeza kasi ya utengenezaji kwa kushirikiana na Watendaji wa Kata ili kuhakikisha zoezi linakamilika kwa wakati.
Dkt Jingu aliwashauri wakandarasi hao kushirikiana na mhandisi ili kuweza kupunguza gharama za nguzo na zoezi la kazi hiyo kukamilika kwa wakati.



More Stories
BAKWATA yawazawadia washindi wakuhifadhi Qur’an
Chalamila:Dar ni salama,aelezea mafanikio na mipango ya maendeleo ya Mkoa
Ulaji vyakula vya aina moja,umri vyatajwa ongozeko la matatizo ya macho Mbeya