December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katibu Jumuiya ya watumiaji Maji Mto Mbarali chini atoa neno

Na David John, Timesmajira Online Mbarali

KATIBU wa Jumuiya ya watumia Maji Mto mbarali chini wilayani humo mkoani mbeya Idrissa Nyahove amesema kuwa amekuwa akipokea vitisho vikubwa ikiwamo kutishiwa maisha Kwa kupitia Imani za kushirikina kutokana na misimamo yake ya kuwazuia baadhi ya wananchi kufanya shughuli za Kilimo kwenye vyanzo vya Maji kwenye Bonde la mto mbarali chini.

Amesema kuwa akiende kwenye mikutano anakutana na maneno magumu kutoka Kwa wananchi wezake huku wengine wakimtaka kuondoka kwenye vikao hivyo lakini vitisho vingine mtu anakuambia kesho uamki lakini kwasababu jukumu lake kubwa nikutunza na kuhifadhi vyanzo vya Maji ataendelea kusimamia Sheria pasipo kujari vitisho hivyo.

Nyahove ameyasema haya Machi 8 wilayani mbarali mara baada ya kutembelewa na kundi la waandishi wa Habari ambao walikuwa wameongozana na wataalamu kutoka Bodi ya Maji Bonde la rufiji iringa .

” Ndugu zangu waandishi kama mnavyoona hapa mwananchi huyu licha ya kuwepo Kwa BIKONi hii lakini mnaona bado ameamua kulima hadi ndani ya mita 60 kutoka mtoni na mwingine yule pale amelima Mahindi hivyo changamoto ni kubwa sana lakini wote hawa tumeshawazuia kutoendelea tena na shughuli hizi .”amesema Nyahove.

Ameongeza kuwa changamoto nyingine ni Kwa wanasiasa na wenyewe wamekuwa ni tatizo sana kwani wanapotekeleza Sheria dhidi ya wananchi wanaovunja Sheria Kwa kufanya uharibifu kwenye vyanzo vya Maji wao wanaingilia Kati kwasababu tu ni wapiga kura wao.

” Kata ya ubaruku wanapata shida sana na wanasiasa lakini wanaendelea kupambana nao japo wao kama Jumuiya msaada wao mkubwa unatoka Kwa watendaji ambao wameajiliwa na Serikali akiwemo mtendaji kata ,polisi pamoja na Mhandisi wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji kidakio cha Great Ruaha Rujewa ,wilayani mbarali Abisai Chilunda.”amesema

Nakuongeza kuwa “Hadi kufikia Sasa wanakesi zaidi ya 30 za watu ambao wameshawachukulia hatua na wengine wamejaza fomu zetu na wamekubari kulipa faini kutokana na uharibifu wanaoufanya na sisi kama viongozi tutaendelea kulinda na kuhifadhi vyanzo vya Maji na hili ndio jukumu letu kubwa sana.”amesema Nyahove.

Nyahove amefafanua kuwa licha ya uharibifu wanaoufanya lakini Sasa wanaendelea na mchakato wa upandaji miti katika maeneo hayo ya pembezoni Bonde la Mto mbarali chini lengo likiwa ni kuhifadhi na kutunza mazingira huku wakiendelea kuwazuia wananchi kufanya shughuli zao kwenye Bonde hilo.

Pia amesema kuwa wataendelea kusimamia Sheria na kwakweli katika hilo wanashukuru sana uongozi wa Serikali ya kata kwani wamekuwa wakipata msaada mkubwa sana hasa kutokana na vitisho wanavyokutana navyo.

Nyahove amesema katika nafasi yake hiyo kwenye Bonde hilo la mto mbarali anasimamia katika vijiji sita na amekuwa akipata ushirikiano mkubwa sana kutoka Kwa Serikali na mhandisi wa Bodi ya Maji Bonde la Rufiji Great Ruaha Rujewa wilayani humo Abisai Chilunda.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Bodi ya Maji Bonde la Rufiji Iringa Pendo Rugalla amesema Jumuiya hiyo ya watumiaji Maji ipo inafanya kazi zake Kwa mujibu wa Sheria na kwakweli wanakazi kubwa sana ya kulinda na kuhifadhi vyanzo vya Maji.

Amesema kuwa wamekuwa wakikutana na changamoto kubwa kama anavyo sema Katibu wa Jumuiya ya watumia Maji Bonde la mto mbarali chini na kama Jumuiya hizo zisingekuwepo hali ingekuwa mbaya zaidi kama tu jumuiya zipo lakini bado wananchi wanaingilia vyanzo vya Maji.