May 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

LSF yashiriki na kuwezesha Kongamano la Kitaifa la Wanawake

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

Mwaka wa pili mfululizo, LSF imeshiriki na kuwezesha Kongamano la Kitaifa la Wanawake lenye lengo la kujadili tafiti mbalimbali zilizofanyika katika masuala ya wanawake ili kubaini hali halisi na kuweka mipango mikakati katika kushughulikia masuala ya wanawake katika nyanja ya kiuchumi, kijamii, na kisiaasa kwa ajili ya kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Akizungumza wakati wa kongamano hilo, Meneja Rasilimali na Mawasiliano LSF, Jane Matinde amesema Haki Yangu App itasaidia kuendana na ubunifu wa teknolojia na kuwawezesha wanawake na wasichana kijamii na kiuchumi lakini pia kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria na upatikanaji wa haki kwa wote.

“Katika kuendana na ubunifu wa teknolojia ili kuwawezesha wanawake na wasichana kijamii na kiuchumi na kuhakikisha huduma za msaada wa kisheria na upatikanaji wa haki kwa wote, LSF tumezindua Haki Yangu App inayowezesha kupata elimu ya kisheria, kupata huduma za msaada wa kisheria , kutoa mafunzo maalumu kwa wasaidizi wa kisheria. Kupitia Haki Yangu App, kesi takribani 315 zikiwemo za unyanyasaji wa kijinsia, migogoro ya ardhi, mirathi, migogoro ya ndoa, matunzo kwa watoto zimeripotiwa na kufanyiwa kazi.” Amesema Matinde

Pichani ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha, Emmanuela Kaganda Mtatifikolo, akimkabidhi Meneja wa Rasilimali na Mawasiliano wa LSF, Jane Matinde, cheti cha shukurani ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa LSF katika kuwezesha Kongamano la Mwaka la Wanawake kwa 2023 lililoandaliwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum chini ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa kushirikiana na LSF pamoja na wadau wengine.
Meneja Rasilimali na Mawasiliano LSF, Jane Matinde
Wadau wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake Mwaka 2023 lililoandaliwa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum chini ya Chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru kwa kushirikiana na LSF na wadau wengine wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kongamano hilo leo Jijini Arusha.