December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Katambi awataka vijana kumuunga mkono Mbunge Bonnah

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi, amewataka VIJANA Jimbo la Segerea kulindwa ili wawe nguvu kazi la kesho kwa kuwa Wazalendo na nchi yao.

Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Patrobas Katambi,alisema hayo leo katika Bonanza la Michezo katika mashindano ya Bonah Cup Jimbo la Segerea Viwanja vya Kinyerezi Wilayani Ilala leo.

“Serikali ina Jukumu la kusimamia vijana wake na kuakikisha vijana wanalindwa kwani vijana wasipolindwa uwezi kupata vijana wazuri wa baadae” alisema KATAMBI.

Naibu Waziri KATAMBI alisema vijana wana wajibu wa kujua makuzi yao na kusikiliza matakwa yao na fursa kwa vijana kuwapa kipaumbele waweze kukua kizalendo kupenda Taifa lao .

Alimpongeza Mbunge wa jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli kuanzisha mashindano hayo kuwaunganisha vijana wa Jimbo la Segerea Pamoja pamoja na kushiriki katika michezo kwa ajili ya kujenga mahusiano na kujenga afya .

Aidha alisema Serikali kupitia Chama cha Mapinduzi ina mipango mingi kwa vijana Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli, amefanya mambo makubwa pia hivi Karibuni alisimamisha Bunge dakika 30 kuelezea Miundombinu ya Barabara za Jimbo la Segerea na Sekta ya Elimu kwani ni Mbunge wa pekee mwenye mapenzi mema ya kuwatetea wananchi wake kila wakati jimbo la SEGEREA.

Pia alishauri kuna wajibu wa Vijana wajue UZALENDO wa nchi yao na HISTORIA ya nchi yao na kufatilia mambo yanayofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aliwataka Vijana Jimbo la Segerea kuunga mkono Juhudi za maendeleo zinazofanywa na Mbunge wa Jimbo hilo Bonah Ladslaus Kamoli,ikiwemo sekta ya michezo,sekta ya Elimu na Afya.

Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonah Ladslaus Kamoli alisema katika kuitimisha Bonah CUP 2024 mchango wa Vijana wa JOGNG waliomba kuwezeshwa awali waliomba Viti ili wavikodishe waweze kujikwamua kiuchumi viti vyao wanakabidhiwa leo sehemu ya mradi wao wa kiuchumi ambapo alisema katika jimbo hilo kuna vijana wengi sekta ya michezo.

Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli aliwataka vijana wa Jimbo la segerea kuwa pamoja kushirikiana katika juhudi za maendeleo zinazofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo alisema Ofisi yake wana Ilala wanatambua kazi kubwa anayofanya Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli ambapo alisema Mbunge Bonnah anaunganisha makundi mbalimbali kupitia sekta ya michezo .