Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
KATA ya Kiwanja Cha Ndege jijini hapa,imeungana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuadhimisha siku ya Samia(Dodoma Samia Day)yenye lengo la kueleza mafanikio ya Kata hiyo ndani ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Kaimu Mtendaji wa Kata hiyo,Eunice Mulange amesema kuwa Kata hiyo yamefanyika mambo mengi makubwa katika kipindi hicho ikiwemo maboresho katika sekta ya Elimu ambapo 2020/21 Shule ya Msingi Mlimwa ilipokea kiasi cha Shilingi Mil.24 kwajili ya matundu nane ya vyoo ambayo tayari yameshakamilika na kufanya shule kuwa na matundu 16 kutoka 8 ya awali.

Aidha Mulange amesema madarasa matatu yameongezeka na Mil.70 zimetumika na kufabya shule kuwa na madarasa 26 ambayo yanatosheleza wanafunzi wote.
“Pia Madawati yameongezeka kutoka 500 hadi 878 na kumaliza changamoto ya madawati shuleni hapo,”amesema Mulange.
Vilevile Mulange amesema katika Shule ya Mlimwa B,pia vimejengwa vyumba viwili vya madarasa vyenye gharama ya Mil.32 pamoja na kuongezeka kwa madawati 40 na kufanya kuwepo kwa madawati 284 kutoka 244 ya awali.
Pamoja na mafanikio hayo Mtendaji huyo amesema kuwa Rais Samia amewagusa moja kwa moja wananchi wa Kata hiyo kwa kuvipatia mkopo vikundi 16 wenye thamani ya mil.274,mkopo ambao ni asilimia kumi unaotolewa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa Vijana,walemavu na Wanawake.
Aidha Mulange amesema kuwa Kata hiyo imepata Mradi wa Mabomba Makubwa ya kutoa taka moja kwa moja kwenye nyumba za watu hivyo wananchi wa Kata hiyo sasa hawachimbi Makalo,mradi ambao umegharimu bil.4.9 fedha kutoka Serikali kuu.
Akizungumza katika maadhimisho hayo Shekhe wa Kata hiyo Mahmoud Nkusa ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi amesema kuwa ili kuendelea kuayaona maendeleo yanayofanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan wananchi wanatakiwa kulinda amani ya nchi kuelekea uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.


Amesema kuwa Rais Samia amefanya maendeleo mengi katika kata hiyo na wananchi wanayaona lakini kusipokuwa na amani hivyo vyote havitaoneka kwasababu hakutakuwa na elimu wala kazi.

“Nasisitiza kulinda amani kwasababu ndiyo msingi wa kila kitu ikiwemo maendeleo haya tunayo ya shuhudia leo wapo wenzetu nchi jirani wanatamani kuja kuishi Tanzania kwasababau ya amani tuliyonayo hivyo tujitahidi kuilinda,”amesema Shekhe Nkusa.
Awali mlezi wa Kata hiyo(CHRO),Francis Kilawe amesema kuwa Miradi iliyofanywa katika kata hiyo imewakutanisha wananchi moja kwa moja na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwani hata wasipomuona wao wataona miradi na watakuwa wamekutana naye kwa namna ya kutumia miradi hiyo.
Huku Diwani wa Kata hiyo Amos Mbalanga akisisitiza kulindwa kwa miradi hiyo kwani ndiyo alama ya kiongozi huyo katika Kata hiyo.
Maadhimisho hayo yameadhimishwa katika kata hiyo kwa kutanguliwa na zoezi la upandaji miti kwenye eneo lilipo Ofisi hiyo na kuudhuliwa na Viongozi mbalimbali wa Kata hiyo,Wakiwemo watendaji wa mitaa,wenyeviti wa Mitaa,Wazee Mashuhuri,Walimu,Wanafunzi na wananchi wa Kata hiyo.






More Stories
Yas yaja na ‘Anzia Ulipo’ kuhamasisha watanzania kusimamia ndoto zao
Coca-Cola Kwanza kuwanufaisha mama lishe Stendi ya Msamvu Marogoro
Sheikh Ponda akabidhiwa kadi ya heshima ya Maalim Seif