Na Mwandishi wetu, Timesmajira Online
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti (SBL) kupitia bia yake ya Pilsner Lager imefanya droo ya kwanza ya promosheni yake pendwa ijulikanayo kama ‘Kapu la Wana’ kubainisha washindi wa kwanza wa promosheni hiyo ambayo ni maalumu kwa wateja wa bia kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini.
Kupitia promosheni hiyo inayofanyika kwa muda wa wiki 8, wateja wa bia ya Pilsner watajishindia zawadi mbalimbali zikiwemo, televisheni, simu janja, pikipiki na zawadi ya mwisho ya gari.
Droo imefanyika na kupatikana washindi 7 kutoka kanda zote tatu, ambapo mshindi mmoja kutoka kanda ya Ziwa alishinda pikipiki, wengine watatu kutoka kanda zote tatu walishinda simu janja na wengine watatu walishinda televisheni.
Washindi hao wanatarajiwa kukabidhiwa zawadi zao tarehe 18 mwezi huu.Washindi walioshinda simu janja ni Agatha Mvwango, Eli Elias na Hassan Joel; waliojishindia television za kisasa ni Justine Mwaipaja, Neema Abdallah na Selina Panga. Na mshindi wa bodaboda ni Neema Mathias kutoka kanda ya Ziwa.
Akizungumza wakati wa droo hiyo, Meneja wa bia ya Pilsner, Wankyo Marando alisema, droo hiyo ni mwanzo tu wa promosheni ya ‘Kapu la Wana’, akitoa wito kwa wateja wa bia ya Pilsner mikoa ya kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini kuendelea kushiriki kwenye promosheni hiyo kwani zawadi ni nyingi.
“Kupitia promosheni hii tunawazawadia wateja wetu wachapa kazi, na zawadi zipo nyingi sana hivyo nawatia moyo wateja wetu wa mikoa ya hizi kanda tatu, yani kanda ya Ziwa, Kusini na Kaskazini waendelee kununua bia ya Pilsner, wapate kadi ya kukwangua, wakipata namba wataituma kupitia ujumbe mfupi wa maneno (SMS) kwa namba 15320 baaada ya hapo watapokea ujumbe mfupi kudhibitisha ushiriki,“ alisema Marando.
Kwa upande wake, Muwakilishi kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha ya Tanzania, Salim Mgafi aliwapongeza washindi wa droo hiyo ya kwanza kwa njia ya simu, na pia alipongeza kampuni ya bia ya Serengeti kwa kufanya promosheni kwa kufuata kanuni na taratibu za bodi ya Michezo ya kubahatisha.
Hii ni mara ya pili bia ya Pilsner imekuja na promosheni hii ya ‘Kapu la Wana’ na imetenga zaidi ya Tsh. 36 milioni kwa washindi 22 wa kampeni hiyo.
More Stories
Waziri Jerry afanya uteuzi wa Makamu Mwenyekiti, Wajumbe watano wa bodi ya Shirika la Posta
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa