Kiungo kiraka Deus Kaseke amesema baada ya changamoto nyingi walizopitia msimu uliopita, msimu huu wamejipanga kufnya vizuriKaseke ambaye amepewa majukumu ya unahodha wakati huu akisubiriwa kocha mkuu, amesema kwa upande wake atahakikisha anaisaidia timu kufikia malengo
“Msimu mpya mara nyingi unakuwa na changamoto nyingi maana kila timu hujipanga kutokana na ushindani uliopo, nasi tumejipanga kuhakikisha tunafanya vizuri”
“Binafsi, namuomba sana Mungu anisaidie maana natarajia kufanya vyema zaidi ya nilivyofanya msimu uliomalizila ili kuipa mafanikio timu yangu nje na ndani ya uwanja,” alisema KasekeKaseke ni mmoja wa wachezaji waandamizi waliobaki kwenye kikosi cha Yanga, pamoja na nyota kama Haruna Niyonzima na Said Juma Makapu
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania