Na Mwandishi Wetu,Timesmajiraonline
NAIBU Waziri wa Nishati Judith Kapinga ameshiriki Jukwa la Mawaziri (Ministerial Symposium)nchini Afrika Kusini ikiwa ni sehemu Kongamano la Wiki ya Mafuta Afrika (Afrika Oil Week) linalofanyika Jijini Cape Town.
Lengo la jukwaa hilo ni kutangaza fursa za uwekezaji kwenye Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala
Jukwaa hilo pia limehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Dkt. James Mataragio, Kamishina wa Petroli na Gesi Goodluck Shirima na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mkondo wa Juu wa Petroli ( PURA), Mha. Charles Sangweni.
Maudhui ya Kongamano hilo ni pamoja na kutangaza fursa za uwekezaji katika miradi ya Mafuta, Gesi Asilia na Nishati Mbadala katika Bara la Afrika.
Kongamano hilo litamalizika tarehe 10, Oktoba, 2024 nchini humo.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais