December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni zaja na bima ya mahusiano

Mkuu wa idara ya utunzi na malezi wa mtalimbo books Mwamwingila Goima kushoto akieleza programu ya bima ya mahusiano na riwaya yake iliyokuwa imeandaliwa na Kampuni yake huku kulia kwake ni mkurugenzi wa Dhahabu publisher Hussein Wamaywa ambaye wameshiriki katika kuandaa programu hiyo.

Na Bakari Lulela, Timesmajira Online DSM

KAMPUNI ya kitanzania ya mtalimbo books ya Dar es salaam kwa kushirikiana na Dhahabu publisher wameandaa program ya bima ya mahusiano ambayo ni mkombozi kwa Taifa.

Akizungumza jijini katika mahojiano na chanzo cha habari hizi mkuu wa idara ya utunzi na malezi wa mtalimbo books Mwamwingila Goima amesema bima hiyo ni rafiki na ni mkombozi kwa Dunia.

“Programu hii ya bima ipo kwa lengo la kujenga mahusiano bora ya kimapenzi Ili yasibomoke ndani ya jamii zetu na kuhakikisha yanakuwa endelevu kwa wawili wapendanao,” amesema Mwamwingila

Aidha Kampuni hiyo imejikita zaidi katika kubuni wazo ya kazi za fasihi na kuendelea wazo hilo Ili kuwa katika kitabu kwa nakala ngumu au laini ambapo wameandaa riwaya ya bima ya mahusiano Ili iwe saidizi kwa Dunia.

Mwamwingila ameeleza kupitia Kampuni yake Kuna miradi ya aina tatu ambayo hushughulika nayo ikiwemo usimamizi wa waandishi wa riwaya , wahariri wa kazi za fasihi pamoja na kazi za kijamii.

Kwa upande wake mkurugenzi wa Dhahabu publisher Hussein Wamaywa amesema lengo kuu la programu hiyo ni kuisaidia jamii kuishi kwa usalama huku ikitambua kujisomea vitabu ni sehemu ya maisha na kikubwa ni kuona hisia na mitazamo inaelekezwa kwenye kuyalinda mahusiano.

Hata hivyo mkuu huyo ameeleza Dhahabu publisher wameshiriki katika kuandaa riwaya ya bima ya mahusiano lakini kazi wanazozifanya ni pamoja na kuandaa matamasha mbalimbali,kuendesha miradi ya watoto pamoja na watu wazima.