December 31, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya Xerin Logistics yaishukuru Serikali ya Tanzania

Na Jackline Martin, TimesMajira Online

Kampuni ya usafirishaji mizigo kutoka nje ya nchi kuja nchini Tanzania, Xerin Logistics Limited waneishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara hasa wasafirishaji mizingo.

Hayo yalisemwa Agosti 21, 2024 na Afisa uendeshaji kutoka kampuni hiyo, Idarous Yussuf, katika Tamasha la Kariakoo Festival lililofanyika Jijini Dar es Salaam, ambapo kampuni hiyo imeshiriki ili waweze kuwafikia wafanyabiashara wengi ambao wanasafirisha mizigo yao.

“Tunaishukuru serikali ya Tanzania chini ya Rais Dkt. Samia kwa kutuwekea mazingira mazuri kwa sisi wafirishaji wa mizigo” Alisema 




Alisema Kampuni yao wanasafirisha
Mizigo kwa njia ya ndege inayotumia siku mbili, na njia ya meli inayotumia siku 20.

“Tunasafirisha mizigo mikubwa na midogo pia mfano magari, kontena, spea, nguo n.k  ambapo kwa ndege inatumia siku 2 na meli inatumia siku 20 mpaka kufika Tanzania”

Aidha alisema mbali na kuwepo kwa kampuni mbalimbali za usafirishaji mizigo kutoka nje, wao kama Xerin wamejitofautisha
Kwa kuwawezesha wafanyabiashara kuwakutanisha na wauzaji bidhaa kutoka nje ya nchi lakini pia kuhakikisha mizigo yao inakua salama tangu inapoagizwa hadi kufika nchini.

“Utofauti wetu na wengine sisi tunaweza kumuunganisha mfanyabiashara na wasambazaji bidhaa waliopo dubai, pia tunamfumo wa kumuwezesha
Mteja mzigo wake kuanzia ulipo, ulipofikia mpaka ulipofika Tanzania”