January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni ya Toyota Tanzania na AFROIL zaingia makubaliano kusambaza vilainishi bora nchini

Na Jackline Martin,TimesMajira Online

kampuni ya Toyota Tanzania Limited kwa kushirikiana na kampuni ya uuzaji wa vilainishi ya AFROIL Tanzania wameingia makubaliano ya kibiashara ya kusambaza vilainishi vyenye ubora vilivyoenea nchi nzima

Lengo ni kuhakikisha mteja anapata Oil za Toyota pamoja na mafuta na huduma nyingi zinazotolewa na AFROIL katika vituo vyao vya mafuta nchini

Akizungumza na waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo (Juni 7 2022), Meneja wa Vilainishi Toyota Tanzania Limited, Anam Mwemutsi amesema ili kuboresha kiwango cha utendaji imara wa injini za Toyota kunahitajika kufanyika huduma mara kwa mara;

“Injini za Toyota zimeundwa kwa hali ya juu na ina utendaji imara kwa muda mrefu na kwa kiwango cha juu hivyo ili kudumisha kiwango hichi inahitajika huduma ifanyike mara kwa mara na kutumia vilainishi bora vinavyoendana na injini”

Aidha Mwemutsi amesema Toyota Tanzania imechagua kufanya kazi na AFROIL kwasababu ni kampuni inayokuwa kwa haraka na yenye lengo la kuweka uwekezaji mkubwa hapa nchini ikiwa imejipanga kutoa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu na huduma nzuri kwa wateja wote hapa nchini.

Amesema vilainishi hivi vya TGMO vimetengenezwa mahususi kwa kuzingatia viwango Vya magari ya Toyota ili kuhakikisha injini kufanya kazi kwa ubora wa hali ya juu

Pia Mwemutsi ameyataja manufaa kadhaa kwaajili ya injini ya Toyota ikiwemo Ulinzi, nguvu, uchumi, Kuegemea, Urefu wa maisha, na Utangamano.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa AFROIL, Lufti Binkleb, amesema muungano huo utasaidia kuboresha hali ya matumizi ya wateja kwa kutoa mafuta ya hali ya juu na vilainishi vilivyo bora;

“Muungano huu unatupa fursa ya kuwahudumia wateja wetu vizuri zaidi kwani sasa vituo vyetu vimekuwa vinatoa huduma tofauti tofauti na kuleta urahisi kwa wateja wetu lakini pia huduma na bidhaa zote zinazopatikana sehemu moja, lengo letu ni kuboresha hali ya matumizi ya wateja wetu kwa kutoa mafuta ya hali ya juu na sasa vilainishi vya ubora vilivyo chini ya paa moja ili kuhakikisha kuwa injini za magari zinafanya kazi kwa ubora wake”

Naye Meneja Masoko wa AFROIL Erasmo Nyoni amesema lengo lao ni kuhakikisha kuwa injini za magari zinafanya kazi kwa ubora wake;

“Muungano huu unatupa fursa ya kuwahudumia wateja wetu vizuri zaidi kwani sasa vituo vyetu vimekuwa vinatoa huduma tofauti tofauti na huleta urahisi kwa wateja wetu na pia huduma na bidhaa zetu zinapatikana katika sehemu moja”

Erasmo amesema kupitia ushirika huo wameendelea kuimarisha vituo vyao na kurahisisha upatikanaji wa huduma kwenye eneo moja.

Pia Erasmo amewataka wateja wote kuweza kupata vilainishi bora vya Toyota Genuine Oil (TGMO) kutoka kwenye vituo vyao ambavyo vinafanya kazi masaa 24.

Kampuni ya Toyota Tanzania imekuwa msambazaji aliyeidhinishwa wa Toyota Motor Vehicles and Genuine Parts nchini tangu mwaka 1965 ambapo katika kupanua wigo wa bidhaa sasa Toyota Genuine Motor Oli
(TGMO) inakuja katika aina 3 tofauti ambazo ni 5W-40 na 20w-50 ambapo inapatikana katika mtandao wa wauzaji wa Toyota Tanzania na vituo vyote vya mafuta ya AFROIL