Na Penina Malundo,TimesMajira,Online
MIONGONI mwa Changamoto zinazowakabili wafanyabiashara wengi wanaoingiza magari nchini ni pamoja na uwekaji wa mafuta machafu ambao unaoathiri mfumo wa injini katika magari mengi na kusababisha gari kuonekana bovu.
Akizungumza hayo mwishoni mwa wiki Jijini Dar es Salaam,Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Magari aina ya Nissan Tanzania,Mark Van Rooyen wakati wa uzinduzi wakati wa uzinduzi wa gari mpya aina ya Navana SC yanayoingizwa na kampuni hiyo ya Nissan .
Amesema mara nyingi magari yanapoingia nchini yanakuwa hayana itilafu ila nafuta yanayowekwa katika magari hayo yanakuwa ni miongoni mwa Changamoto ya kusababisha ubovu katika injini.
Rooyen amesema gari hilo jipya lililozinduliwa ni miongoni mwa magari yao ambayo yanafaa katika shughuli mbalimbali hususani zile za kubeba mizigo.”Hii gari ni jipya nchini na sisi ndo wa tuliochelewa kuliingiza nchini tayari nchi kama Kenya ilishaingiza gari kama hilo ni miongoni mwa magari mazuri ambayo ni imara na ni mazuri katika kutumia hasa shughuli za kubebea mizigo,”amesema na kuongeza kuwa
“Mwaka huu tumeleta gari hili ambapo bei yake ni Milioni 63 ambapo tutatoa services ya gari bure kwa miaka miwili na tunatoa dhamana ya miaka mitatu kwa mtu atakaenunua gari hiyo,”amesema
Aidha amesema gari hilo lililozinduliwa ni la kwanza kuwepo hapa nchini hivyo aliwaomba watanzania kuchangamkia fursa ya kununua gari hilo kwani ni la viwango vya juu
Rooyen amesema kampuni hiyo imekuwa ikitengeneza magari yenye ubora wa kukidhi viwango vya juu ambapo pindi mtu anapotumia magari hayo hawezi kununua mara kwa mara.
“Leo tunazindua gari aina ya Nissan Navara SC ambapo gharama zake ni nafuu kila mtanzania anauwezo wa kumudu, na kumuwezesha kufanya shughuli zake kutokana na kuwa na ubora halisi “amesema
Kwa upande wake, Meneja Masoko na Mauzo wa Kampuni hiyo, Alfred Minja amesema kampuni hiyo imekuwa ikifanya Mapinduzi makubwa katika Sekta usafirishaji kwa kutengeneza magari ambayo yanaubora wa kutosha.
Amesema kutokana na matumizi ya kila siku gari aina ya Nissan Navara SC itamsaidia muhusika kusafiri salama na kufanya kazi zake bila wasiwasi aina yoyote.
“Kupitia usafiri huu wa gari aina ya Nissan Navara SC mtumiaji atapata fursa kufanya shughuli zake kwa ubora pasipo kuwa na wasiwasi wa aina yoyote kwani imetengenezwa kwa ubora wa hali ya juu”amesema
More Stories
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi
Kampeni ya Sako kwa Bako yawafikia Kanda ya Kati