Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Kampuni ya Gf Truck & Equipments Lt Kupitia kampuni yake ya ukodishaji wa mitambo ya RENTO MACHINE wameingia wamesaini makubaliano na shilika la madini nchini Stamico kwa ajili ya kuwasaidia na kuwainua wachimbaji wadogo wa madini ili kuweza kuongeza pato lao na pato la taifa kwani kwa kufanya hivyo kutaongeza morali kwa wachimbaji wadogo ambao hawana uwezo wa kununu mashine hizo za kuchimbia.
Gf Trucks & Equipment’s ambao ni wauzaji wa mitambo ya kuchimbia ya XCMG na AJAX wanautaratibu wa kuwakopesha wakandarasi wadogo wa miradi mbali mbali ya serikali kwa dhamana na mtambo husika kupitia beki rafiki ambayo Mkandarasi mwenye mradi anaweza akakopesha vitendea kazi na akalipa kwa awamu.
Akizungumza wakati wa kusaini makubaliano hayo mkurugenzi wa Masoko na mawasiliano wa kampun ya GF Salman Karmali alisema wao wamegundua kwamba wachimbaji wengi wadogo hawana mitaji ya kuweza kununua mitambo hiyo na kutokana na hilo wameamua kuingia makubaliano na Stamico ya kuwakodisha mitambo maalumu ya kuchimbia kwa dharama nafuu Satamico kama walezi wa wachimbaji madini nchini ni rahisi kumtambua muhusika mwenye mahitaji na kwa kufanya hivyo tutapunguza ajali nyingi zinazotokea migodini kwa wachimbaji kutumia njia za asili na sasa tumekuja kama mkombozi wao kupitia XCM na AJAX tutakua tumetatua changamoto zao kwa kiwango kikubwa.
Akizungumza kwa niaba ya wachimbaji wadogo mmoja ya mchimbaji katika mgodi wa Chunya mkoani Mbeya ,Naumu Mwakasita alisema wao wameichukulia hii kama ni fursa inayokuja kuwakomboa na hali ya kutumia vifaa duni katika uchimbaji hivyo yeye atakuwa mtu wa kwanza kuchangamkia fursa hii na kuachana na uchimbaji kwa kutumia njia za asili ambazo ni hatari
Nae Waziri wa madini Dotto Biteko aliwataka kuchangamukia furusa ya kutumia mitambo hiyo na kuacha kuchimba jambo ambalo litaongeza thamani ya madini na kuweza kupata madini yenye ubora itakayopelekea kuuza madini yetu kwa thamani kubwa
“Ninazo taarifa wachimbaji wengine wamekuwa wakichanganya na vitu vingine ili kuongeza uzito, mfano unachimba gympsum umeshaipata lakini unaamua kuchukua mchanga usiokuwa na thamani yoyote ili kuongeza uzito wa mzigo wako,” alisema Dk Biteko.
Alisema kwa kufanya hivyo wamekuwa wakiwatia hasara wenye viwanda jambo ambalo linaweza kuwafanya kufirisika, kufunga viwanda na kuwafanya wao kama wachimbaji wakose soko.
“Kuweni waaminifu, kama hauiogopi serikali basi muogope Mungu, hakuna mtu mwenye akili yake timamu anayeweza kuagiza malighafi kutoka nje kama hiyo malighafi anapata hapa nchini kwa bei nafuu na safi, wakati mnawalalamikia wenye viwanda kuwapunja nanyi zalisheni zalisheni bidhaa zenye ubora,” alisema Biteko.
Hilo lilibainika baada ya kuwapo kwa malalamiko kutoka kwa wachimbaji wakieleza kupunjwa fedha na wenye viwanda kwa kukatwa baadhi ya tani na wanunuzi kwa kuhofia kuwa zitakuwa na takataka.
“Kama mtu amepeleka gari lake la tani 30, tani 3 zinakatwa na kuhesabiwa kama ni uchafu, wanampunja mchimbaji kuanzia kwenye uzito na wakati mwingine katika kutumia bei elekezi.
Alisema ni vyema kuwapo kwa ushirikiano thabiti kwani sekta ya madini ya viwandani ni moja kati ya zinazokuwa kwa kasi, ndani ya miaka miwili ya Rais Samia Suluhu Hassan, mapato yake yamefikia Sh1.19 trilioni kutoka Sh456 milioni.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba