March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampuni 15 zavutiwa  kuwekeza  Kongani ya Buzwagi

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

MKUU wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita amesema kuwa Mkoa huo umefanikiwa kuanzisha Kongani maalumu ya Uwekezaji na hadi sasa Kampuni 15 zimeonesha nia ya kuwekeza katika Kongani maalumu ya Uwekezaji(SEZ) ya Buzwagi.

Amesema  mpaka sasa kampuni moja ya East Africa Conveyers Service imeanza uzalishaji na Kampuni nne zimeanza taratibu za kupata Leseni na zimefanya usajili wa Mradi NEMC.

Mboni amesema hayo jijini hapa leo Julai 14,2025 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio ya miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita.

Amesema kuwa Kongani hiyo itakuwa ya kipekee kutokana na kuwepo kwa miundombinu ya kisasa ikiwemo kituo cha kuzalisha umeme kwa matumizi ya ndani ya eneo hilo.

Aidha amesema kuwa Mkoa huo umeanzisha Viwanda vikubwa 4 kutoka 36 mwaka 2020 hadi 40 mwaka 2025,viwanda vya kati 12 kutoka 180 hadi 192 mwaka 2025 na viwanda vidogo 222 kutoka 999 mwaka 2020 hadi
viwanda 1,225 mwaka 2025.

Vilevile amezungumzia Mafanikio yaliyopatikana katika usimamizi wa sekta ya madini ambapo amesema uzalishaji wa madini umeongezeka kutoka tani 7.9 mwaka 2020 hadi tani 42.5 mwaka 2025.

Mafanikio mengine amesema ni kuongezeka kwa fedha za kigeni zilizotokana na uuzaji wa madini kutoka Dola za Marekani milioni 44.33 mwaka 2020 hadi Dola
za Marekani milioni 191.15 mwaka 2025;

Kuongezeka kwa mapato ya Halmashauri yatokanayo na uchimbaji wa madini kutoka Shilingi milioni 745.4 mwaka 2020
hadi Shilingi 3,334,265,389.56 mwaka 2025, Kuongezeka kwa masoko na vituo vya ununuzi madini kutoka 06 mwaka 2020 hadi vituo 12 mwaka 2025 na kuongezeka kwa utoaji wa leseni kwa wachimbaji wadogo kutoka leseni 332 mwaka 2020 hadi 1,766 mwaka 2025.

Katika Sekta ya Afya Mboni amesema kuwa
Mkoa huo umepokea shilingi bilioni 79.1 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa
miundombinu ya vituo vya kutolea huduma za Afya.

“Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuimarika kwa miundombinu ya
kutolea huduma za afya, kuongezeka kwa upatikanaji wa dawa, vifaa,
vifaa tiba na vitendanishi na kuimarika kwa upatikanaji wa huduma za
afya karibu na wananchi.

“Mafanikio mengine ni pamoja na Kukamilishwa kwa Hospitali ya Rufaa ya Mwawaza,Kuongezeka kwa idadi ya Hospitali za Wilaya 5 kutoka mbili mwaka 2020 hadi Saba mwaka 2025 katika Halmashauri za
Shinyanga DC, Msalala DC, Ushetu DC, Shinyanga MC na Kishapu DC (Hospitali ya Mwadui).