December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampeni ya “Ni Balaa” yanufaisha jamii

Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online

KAMPENI ya teknolojia na mawasiliano Vodacom Tanzania Plc leo imekabidhi zawadi kwa washindi wa droo ya kwanza ya kampeni yake mpya ya “Ni Balaaa” KilaMtu ni Mshindi, katika viwanja wa Nane Nane jijini Dodoma. 

Kampeni hii inalenga kunufaisha wateja na jamii kwa ujumla, na kuhakikisha kila mshiriki anapata nafasi ya kushinda zawadi, zikiwemo za kila siku, kila wiki, kila mwezi, pamoja na washindi watano wa zawadi kuu.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Joseph Sayi, Mkuu wa Kanda ya Kati wa Vodacom Tanzania, alisisitizamapokezi mazuri ya kampeni hiyo: “Mwitikio kutoka kwawateja wetu umekuwa mzuri sana. Tunafurahi kuona washindiwengi tayari. 

Kila muamala wa M-Pesa wakati wa kampeniunaongeza nafasi yako ya kushinda. Iwe unatuma pesa kwafamilia, unalipia bili, au unatumia M-Pesa super app, kilamuamala unahesabika.”

Kampeni hii, yenye kaulimbiu ya “Kila Mtu ni Mshindi!”, itaendelea hadi Oktoba. Washindi wa kila siku wanapata TZS 100,000, washindi wa kila wiki TZS 500,000, washindi wa kilamwezi TZS 1 milioni, na washindi watano wa zawadi kuu kilammoja atapata TZS 20 milioni, kufanya jumla ya TZS 100 milioni za zawadi. 

Hali kadhalika washindi hawa watanowatapata fursa ya kipekee ya kuchagua shule ambayo Vodacomitasaidia shule hiyo kuboresha mazingira ya kusoma na haswamaktaba.

Mkazi wa Dodoma, aliyetangazwa kama mmoja wa washindi wa kila siku, akiwa mwenye furaha alisema, “Nilishangaa na nafurahi sana kushinda TZS 100,000! Ni ajabukwamba kutumia tu M-Pesa unaweza kuwa mshindi wa zawadinzuri kama hizi. Ninawahimiza kila mtu kushiriki.”

Bw. Sayi aliongeza kuwa kampeni ya “Ni Balaaa” imeundwakuwa shirikishi, ikiruhusu kila mtu kushiriki, bila kujali wapiwalipo au hali zao za kiuchumi. M-Pesa inarahisisha kila mtukushiriki, ikiwemo wamiliki wa biashara ndogo ndogo kutokapopote nchini Tanzania. Kila unapotumia M-Pesa au kununuavifurushi, unaingia moja kwa moja kwenye droo na una nafasi ya kushinda'”.

Kampeni hii pia itanufaisha wamiliki wa biashara ndogo na zakati kila wakijiunga na SME Combo Bundles za Vodacom, hivyo kuwaongezea nafasi ya kushinda zawadi kama mifumo ya usimamizi wa hesabu au kamera kwa ulinzi bora na wa uhakika.