Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
Kampuni inayoongoza Tanzania katika kuhakikisha mtanzania anaishi maisha ya kidijitali Tigo Tanzania, kupitia Promosheni yake ya NDIGA LA KISHUA kwa kushirikiana na kampuni ya HISENSE wametoa milioni nane kwa washindi nane kwa washindi wa WIKI na zawadi ya Vyombo vya ndani ambavyo ni Friji , Spika za mziki (SubWoofer), Smart Tv , pamoja na Microwave kwa washindi wawili wa wiki hii.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi hizo Meneja wa Biashara Tigo Pesa Bi. Restuta Kedmond amesema
” Kampeni bado inaendelea kwahiyo endeleeni kufanya miamala mingi iwezekanavyo kama vile kulipa bili , mikopo ya BUSTISHA , malipo ya kiserikali , kutuma na kupokea pesa kutoka benki n.k kupitia TIGO PESA au piga 15001# ili kuibuka mshindi wa zawadi za pesa taslimu ( milioni 1 kila wiki , Milioni 5 kwa mwezi wa Disemba , na zawadi kuu za pesa taslimu Milioni 10 na Milioni 20 ) , Vifaa vya Ndani vya Hisense na gari jipya kabisa aina ya Toyota Rush “.
Naye Afisa masoko wa kampuni ya HISENSE Bwn.Joseph Mavura amesema kuwa kampuni ya Hisense
Inatoa punguzo la 20% katika maduka yao yote na huduma ya kusafirishiwa bidhaa utakazo nunua hadi nyumbani kwako bure (FREEE DELIVERY), hii ni kwa wateja wote watakao nunua bidhaa kutoka hisense na kulipia kwa njia ya Tigo pesa, pia tunaendelea kutoa vifaa vya Hisense kwa washindi wawili kila wiki
Alimalizia.
Kwa upande wake , mmoja wa Washindi wa Kifurushi cha Bidhaa za Hisense Frola George , amesema kuwa kuwa alipopigiwa simu na kuambiwa kwamba kashinda hakuamini na leo alipofika na kukabidhiwa vifaa vyake ndipo ameamini kwamba wanachokifanya Tigo ni cha ukweli kabisaa
” Nawasihi wateja wa Tigo Pesa waendelee kufanya miamala kwa wingi maana ndio siri pekee ya Ushindi , namimi ntaendelea kufanya miamala maana naweza nikashinda tena milioni zinazotolewa au hata zawadi kubwa kabisa ya gari “
More Stories
Elon Musk : Bill Gates atafilisika endapo…
CRDB yazindua matawi Majimoto, Ilula kuwahudumia wananchi
Lina PG Tour yafufua gofu Moshi