March 29, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kampeni ya chanjo ya polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano yazinduliwa Dodoma

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu amezindua kampeni ya kitaifa ya chanjo ya polio kwa watoto wenye umri wa kuanzia miaka sifuri hadi miaka mitano ili kuepusha kundi hilo la watoto kupata ugonjwa huo huku akiziagiza halmashauri na mikoa yote hapa nchini,kuhakikisha inatoa elimu kwa wananchi ili kuondoa upotoshaji juu ya chanjo ya polio.

Mbali hilo Waziri Ummy amwaagiza  viongozi katika halmashauri na mikoa kuhakikisha fedha zilizotolewa kwa ajili ya kampeni ya ugonjwa wa Polio,zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na siyo vinginevyo.

Takriban asilimia 90 hadi 95 ya wanaoambukizwa ugonjwa huu huwa hawaoneshi dalili zozote, huku asilimia 5 hadi 10 ya watu huonesha dalili hafifu za homa, maumivu ya kichwa, kutapika, kuharisha, mishipa ya shingo kukaza na maumivu katika miguu na mikono huku athari zake zikielezwa kuwa ni mgonjwa kupata ulemavu wa kudumu.

Akizindua kampeni hiyo mkoani Dodoma Ummy amesema  viongozi katika halmshauri mbalimbali lazima wakatoe  elimu kwa jamii ili kuepusha uvumi uliopo miongoni mwa jamii kwamba chanjo hiyo ina madhaa kwa watoto.

“Katika hili,Mkurugenzi wa Afya TAMISEMI naomba mkasimamie,hakikisheni wenyeviti wa vijiji pamoja na viongozi wa serikali za mitaa wanatoa elimu sahihi kuhusu ya chanjo hii  kwa wananch.”amesema Ummy

Halmashauri zote lazima ielekeze fedha hizo kwenye utoaji wa chanjo kwa watoto maana ndiyo kinga yao dhidi yaa ugonjwa huo.

“Ugonjwa wa Polio hauna tiba lakini kinga ipo,nawasihi wazazi na walezi muwapeleka watoto  kupata chanjo hiyo ambayo inamsadia mtoto kutopata Polio akiwa na umri chini ya miaka mitano..,na naomba baada ya uzinduzi huu  mkatekeleze majukumu ya utoaji chanjo katika Zahati,vituo vya Afya,kwa njia ya Tembezi,Mkoba pamoja na kupita nyumba kwa  yumba,”amesema Ummy

Aidha Ummy amesema,baada ya uzinduzi huo wanatarajia kutoa chanjo katika mikoa mikoa 21 ya Tanzania ambapo kwa siku nne za utoaji chanjo hiyo  Serikali imelenga kuwafikia na kuchanja  watoto 10,295,316

“Zoezi la utoaji chanjo hiyo litakuwa la siku nne kwa nchi nzima na huduma zitatolewa katika vituo vya kutoa huduma za afya,ikiwemo Zahati,Vituo vya Afya,Hospitali,lakini kutokana na kufahamu wazazi wanashughuli zao,hivyo zoezi hilo litafanyika kwa njia tembezi na Mkoba ikiwemo kuwafuata maeneo watoto walipo ili kuwakinga watoto,”

Vile vile kwa upande wa Zanzibar  wanalenga kuchanja watoto takribani 281,489 ambapo jumla Bara na Visiwani wanatarajia kuchanja watoto 10,500,000.

Ummy amewataka wazazi na walezi kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo ambao kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani ugonjwa huo upo Msumbiji huku akisema ni vyema watoto wapelekwe kupata chanjo ili kuwakinga dhidi ya polio.

Amewataka wataalamu wa afya kuimarisha huduma za utoaji wa chanjo kwa kipindi chote cha kampeni na baada ya kampeni na kuongeza serikali haijasimamisha utoaji wa chanjo nyingine kwa sababu watoto bado wanazaliwa.

Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka Idara ya Watoto wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wanawake na Makundi Maalum Sebastian Kitiku amesema,suala la afya bora ni miongoni mwa mambo matano ya kuzingatia katika ukuaji wa mtoto hadi kufikia utimilifu wake .

“Ukuaji wa ubongo wa mtoto ni kati  ya umri wa miaka 0-8 ambapo ubongo hukua kwa asilimia 80,kwa hiyo kushindwa kufanya hivyo  ni kutengeneza Taifa lenye watu wasiokuwa na uwezo wa kufikiri,

“Mtoto anahitaji anahitaji afya bora,kwa chanjo ni sehemu ya afya  ili kumjenga mtoto katika suala zima la afya ,pia mtoto anahitaji Lishe bora hii husaidia kufanya ubongo wa mtoto kukua inavyotakiwa ,Ulinzi wa mtoto pia ni muhimu..,hapa siyo kumlinda tu asiumie bali  lakini kufanya yale yote ambayo hayatamuathiri mtoto kisaikolojia ili akue vizuri katika ubongo wake lakini pia kuna suala la Ujifunzaji wa awali wa mtoto pamoja na malezi yenye muitikio,

“Mtoto anapokuwa tumboni mwa mama yake anafanya mawasiliano na mama yake tangu  akiwa tumboni na mara baada ya kutoka anaanza kufanya mawasiliano kutokana na mazingira yanayomzunguka,mzazi anatakiwa kuwasiliana na mtoto na kujua mahitaji yake hata kama hajui kuongea.”amesema Kitiku na kuongeza kuwa

“Maeneo hayo yakitiliwa mkazo  yanaweza kuwakuza watoto na kufikia utimilifu wao kwa maana yao ubongo wao kukua vizuri kwa asilimia 80 na hatimaye kufikia utimilifu wao.”

Amesema,kwa kuzingatia umuhimu wa ukuaji wa mtoto hadi kufikia utimilifu wake ,Serikali  imeanzisha Programu Jumuishi ya Taifa  ya Malezi ,Makuzi na Maendeleo ya Awali ya mtoto kwa lengo la kuhakikisha watoto wa kitanzania wanakua katika utimilifu na hatimaye kupata Taifa lenye kizazi chenye uwezo wa kufikiri na hivyo kuongeza tija katika Taifa.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Antony Mtaka amesema ,koa umepokea dozi 551,209manbapo wanatarajia kuwafikia watoto 479,156 katika halmashauri zote nane.

Mmoja wa wazazi aliyefika na mtoto wake katika uzinduzi huo wa kampeni ya chanjo kitaifa Ashura Mohamed mkazi wa Mailimbili jijini Dodoma ,chanjo ni muhimu kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kwani zimekuwa zikiwasaidia watoto hao katika kuwakinga dhidi ya magonjwa mbalimbali ukiwemo ugonjwa huo wa polio.

.