December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamishna TRA aendelea na ziara Dodoma

Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Msafiri Mbibo akizungumza na Katibu Tawala wa Wilaya ya Mpwapwa Sarah Komba wakati Naibu Kamishna Mkuu huyo alipomtembelea ofisini kwake ambapo alimshukuru kwa ushirikiano unaotolewa na uongozi mzima wa wilaya hiyo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. Picha zote na Veronica Kazimoto
Afisa Msimamizi wa Kodi wa Kituo cha Huduma za Kodi cha Kibaigwa kilichopo chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Mohammedy Madebe akichangia hoja wakati Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Msafiri Mbibo alipotembelea kituo hicho kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi katika ukusanyaji mapato ya Serikali.
Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Mpwapwa Nelson Makweta akiwatambulisha watumishi wa TRA wilayani humo wakati Naibu Kamishna Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw. Msafiri Mbibo alipowatembelea kwa lengo la kuwapa hamasa watumishi hao kuendelea kufanya kazi kwa bidii na weledi katika ukusanyaji mapato ya Serikali.