Fresha Kinasa,TimesMajiraOnline,Mara.
MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini,Mkoa wa Mara Prof.Sospeter Muhongo,ameitisha Kikao cha Kamati ya Mfuko wa Jimbo kwa lengo la kugawa vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa kwa kutumia Fedha za Mfuko wa Jimbo hilo.
Kikao hicho kimefanyika Kijijini Suguti,Makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ambapo Mbunge wa Jimbo hilo Prof. Muhongo amesema kuwa vifaa hivyo vitasaidia kutekeleza malengo yaliyokusudiwa.
Hayo yameelezwa kupitia taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo hilo Januari 7, 2025. Ambapo fedha za mfuko huo zimebainishwa kuwa ni shilingi Mil. 75.796 na vifaa vya ujenzi vitakavyonunuliwa ni Saruji mifuko 1,970, mabati ya rangi 322, nondo,8 mm430.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Waliohudhuria Kikao hicho ni Wajumbe wa Mfuko wa Jimbo, Sekretariati ya Mfuko wa Jimbo,(Wenyeviti wa Serikali za Vijiji vilivyotuma maombi na Wakuu wa Sekondari zilizotuma maombi.
Aidha, orodha ya Sekondari zilizogawiwa vifaa vya ujenzi ni Sekondari zinazojitayarisha kufunguliwa ikiwa ni pamoja na Muhoji, Nyasaungu na Rukuba (Kisiwa).
Pia,Sekondari zinazokamilisha ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi ni
Mtiro,Makojo,Nyambono,Bwai,Mkirira na Etaro na Sekondari zinazoanza ujenzi wa maabara za masomo ya sayansi ambazo ni Bukwaya na Nyanja
“Sekondari mpya zinazoanza ujenzi –
Chitare (Kata ya Makojo), Mwigombe (Kata ya Kiriba), Mmahare (Kata ya Etaro), Musanja (Kata ya Musanja), Kataryo (Kata ya Tegeruka) na Nyabakangara (Kata ya Nyambono)” imeeleza sehemu ya taarifa hiyo.
More Stories
Walimu S/ Sekondari Ilala wafundwa juu ya maadili ya wanafunzi
Dkt. Samia afungua skuli ya sekondari Misufini, Bumbwini
Rais Mwinyi: Barabara Pemba zitajengwa kwa lami