December 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Kamati ya mapendekezo ya wananchi juu ya kumaliza mgogoro wa ardhi tarafa ya Sale,Loliondo na Ngorongoro yakamilisha mapendekezo ya wananchi

Na Mwandishi wetu,timesmajira,online

KAMATI  ya Mapendekezo Tarafa ya Sale, Loliondo na Ngorongoro ya kutatua migogoro ya ardhi ikiongozwa na viongozi wao wa Wilaya akiwemo Mbunge wa Ngorongoro,imetangaza kufika tamati katika kutoa mapendekezo ya wananchi juu ya kumaliza mgogoro wa ardhi tarafa ya sale,loliondo na Nggorongoro.

Taarifa iliyotolewa leo kwa vyombo vya habari na kamati hiyo jana iliyosomwa na  mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo 

Metui Oleshaudo amesema

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa  alikubaliana nao kutumia muda wa wiki mbili kukamilisha mapendekezo hayo.

Kamati amesema mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi kwa vijiji vyote vinavyozunguka eneo lenye mgogoro wa kilometa za mraba 1500 na eneo la mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro umekamilika kama tulivyoeleza awali na taarifa ya maoni hayo inatarajiwa kuwasilishwa kwa Waziri Mkuu Majaliwa pamoja na viongozi wa juu wa serikali pamoja na umma.

“Kamati hii imekutana Aprili 24 na 25, 2022 kukamilisha mchakato huu na itakamilika
wiki hii wakati mchakato huu wa kuandaa mapendekezo ya wananchi ukifikia ukingoni,”amesema na kuongeza

“Baada ya kikao cha mwisho kilichofanyika MSTCDC kamati ya takribani watu 60 kutoka tarafa ya loliondo, Sale na Ngorongoro iliandaa mapendekezo ya wananchi kuhusu mgogoro wa ardhi wa kilometa za mraba 1500 uliopo Tarafa ya Loliondo na Sale na Mgogoro wa Tarafa ya Ngorongoro,”amesema kamati

Aidha kamati hiyo amesema kamati hiyo ya Wilaya ilijumuisha wawakilishi wa Madiwani, wawakilishi wa wenyeviti, wawakilishi wa kinamama, wawakilishi wa viongozi wa kimila (Malaigwanani) na
baadhi ya wasomi wa jamii.

“Tunaishauri serikali kupitia Waziri Mkuu, kukemea vitendo vya ukamataji holela wa
viongozi wakiwemo madiwani, wanajamii, viongozi na watetezi wa haki za binadamu wanaosimama kutetea haki za jamii, pamoja na kuzuia vitisho dhidi ya waandishi wa habari wanaotoa taarifa na maoni ya wananchi kuhusiana na Mgogoro huu,”amesema kamati hiyo