KAMATI ya Usimamizi wa Mradi wa Kukabilina na Vitendo vya Kihalifu katika Bahari na Maziwa Makuu imekutana na kufanya kikao cha dharura kwa lengo la kujadili mkataba wa ununuzi wa boti ya doria litakalosaidia kukabiliana na vitendo hivyo nchini.
Kikao hicho kimesimamiwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo ambaye pia ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. John Jingu katika ukumbi wa ofisi hiyo Mei 30, 2022 jijini Dodoma kikihusisha Makatibu Wakuu kutoka wizara mbalimbali na wadau wa maendeleo.
Miongoni wa wajumbe waliohudhuria ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) Bw. Gabriel Migire, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Abdallah Kirungu, Naibu Mwakilishi Mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mipango ya Maendeleo,Sergio Valdini na Mwakilishi wa Balozi wa Japan Tanzania,Tabuchi Tomoyoshi.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best